Envaya

Envaya

Utafiti wa jamii kuhusu hali ya mafuriko jijini Dar-es-salaam

Respondent: Counselling and Family Life Organization (CAFLO)
Time Submitted: 28 Januari, 2012 10:52 EAT
Miembeni, Vingunguti
Maji safi, miundo mbinu mizuri, elimu ya afya na utunzaji wa mazingira.
Mafuriko yaliyotokea yameongeza ugumu wa maisha kutokana na kwamba mali nyingi zimepotea kutokana na mafuriko, kwa mfano mimi nimepoteza vyombo vya ndani, vyakula (maharage, unga, mchele), mifugo (kuku) vyote vilisombwa na mafuriko.
Kusema kweli mafuriko haya yamenirudisha nyuma kimaendeleo kutokana na kwamba nimepoteza viti vingi sana kama ambavyo nimeshaeleza. Kwa hiyo kiwango cha umasikini kwa sasa kimeongezeka.
Huduma ya maji baada ya mafuriko limekuwa na changamoto nyingi kutokana na uharibifu wa miundo mbinu kwa maana kwamba watu wa mtaa huu walikuwa wanategemea zaidi maji ya visima, lakini baada ya mafuriko hayo visima vingi vimeharibika ambapo vilivyokuwa na matenki baadhi ya matenki hayo yaling`olewa na mafuriko.
Kabla ya mafuriko: dakika 30Sasa: dakika 30
(Hakuna jibu)
« Jibu lililotanguliaJibu lifuatalo »

« Rudi nyuma kwenye ripoti