Respondent: | Counselling and Family Life Organization (CAFLO) |
---|---|
Time Submitted: | 28 Mutarama, 2012 at 15:55 EAT |
Mtakuja bondeni, Vingunguti.
Viongozi wa serikali waje kutengeneza mifereji mikubwa ya kupitisha maji, maana eneo hili halina njia maalum ya maji, hivyo mvua ikinyesha lazima maji yatwame na kama ni nyingi ndipo mafuriko hutokea.
Nyumba ambayo tulikuwa tumepanga imeharibika vibaya, vilevile vitu vya ndani karibu vyote vimeharibika, kwa hiyo ni maafa makubwa.
Kwanza mafuriko hayo yamepoteza vitu vingi vya ndani na vingine vimeharibika, nimepoteza radio, TV, nguo, vyombo vya kupikia na kulia, vitanda na magodolo havifai kwa sasa, vifaa vya shule vya watoto wangu vimeharibika, hivyo mafuriko haya yameleta matatizo makubwa katika maisha yangu, hali imekuwa mbaya, maana sina uhakika kuwa hata watoto wangu watarudi shuleni.
Maji kwa ujumla siyo mazuri, kutokana na kwamba mafuriko hayo yaliharibu visima vingi hapa kwenye mtaa wetu, kiasi kwamba sasa hivi inatubidi kwenda masafa marefu kwa ajili ya kutafuta maji.
Before flooding: dakika 25 | Now: dakika 25 |
(No Response)
« Back to report