Respondent: | Counselling and Family Life Organization (CAFLO) |
---|---|
Time Submitted: | January 25, 2012 at 10:41 PM EAT |
Mtaa wa Kombo, kata ya Vingunguti.
Kwa sasa mtaa unahitaji sana kuwe na mifereji au njia za kupitisha maji, maana hakuna mifereji ya maana inayoweza kupitisha maji kwa urahisi na kuweza kuzuia mafuriko yasitokee.
Kwa ujumla mafuriko yameleta maafa makubwa sana katika familia yangu, maana nimepoteza vitu vyote vya ndani mfano vyombo vyote, vitanda, nguo, vilevile hata nyumba yetu imeweza kuharibika kwa kupata nyufa nyingi zinazotokana na kujaa maji mengi.
Kwa ujumla mafuriko haya yameongeza sana kiwango cha umasikini katika maisha yangu, maana mali zangu zote zimepotea, hata pesa ambazo nilikuwa nazo zipatazo laki tano ziliweza kuchukuliwa na maji, maana siku ile mafuriko yanatokea pesa hizo nilikuwa nimeziweka kwenye kabati ya meza ambapo nilikuwa nimepanga kuzitumia siku inayofuata kwa ajili ya kununulia biashara yangu huko kariakoo, lakini kwa bahati mbaya zimetwaliwa na maji, sasa sijui nitafanya nini.
Nidhahiri kuwa maji tunayotumia kila siku yameathirika kwa kiasi kikubwa, kutokana maji tunayotumia niya visima vilivyochimbwa, hivyo mafuriko haya yameweza kuharibu visima hivyo na kuweza kuchafua maji hayo, na kuweza kupoteza ile thamani ya kuwa maji ya kutumia katika familia.
Before flooding: dakika 45 | Now: dakika 45 |
(No Response)
« Back to report