Maoni kuhusu Utekelezaji wa Sensa kwa Mwaka 2012
Hili ni zoezi la nne la sensa ya watu na makazi tangu kupatikana kwa uhuru wa Tanzania mwaka 1961. Sensa hii hufanyika baada ya miaka kumi kama utaratibu ulivyo tangu kuanza kwa zoezi hili. Kwa mwaka huu zoezi lilianza tarehe 26/08/2012 kwa nchi nzima. Umuhimu wa zoezi hili ni kujua idadi ya watanzania na makazi yao ili serikali iweze kupanga mikakati yake ya maendeleo.
Kabla ya serikali kuanza kutekeleza zoezi hili tulisikia juu ya kugoma kwa makalani kutokana na kwamba walicheleweshewa malipo ya posho zao kama yalivyokuwa mapatano yao na serikali, pia tulisikia migomo mbalimbali kutoka kwa raia, viongozi wa dini na wenyeviti wa vijiji katika kona mbalimbali za nchi kwa madai ya kutoshiriki zoezi la sensa.
Kufuatia hayo yote, Envaya kama shirika la kijamii liliamua kufanya utafiti ili kujua utekelezaji wa mchakato mzima.
Soma majibu yao, na kutoa maoni yako!