Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

POSHO ZA WABUNGE NA KEKI YA TAIFA

Community Empowerment Foundation (COEF) (Kigamboni, Dar es Salaam)
June 15, 2011 at 2:16 PM EAT

Wabunge wa kambi ya upinzani wamependekeza posho za vikao vya wabunge zikatwe ili pesa itakayokatwa iwekwe kwenye kasma nyingine za miradiya maendeleo. Makada wa CCM, wabunge na Spika wao hawataki posho hizo ziguswe. Wnasahau yafuatayo:

1. Kulipwa mara mbili kwa kazi ileile ni ufisadi.

2. Kipatao wanachokipata kutokana na posho za vikao hakikatwi kodi, na huu ni ufisadi.

3. Posho wanazopata ni kubwa zaidi kuliko mishahara ya watumishi wengi.

Wanaharakati tutafakari haya mambo tukiweka maanani kwamba Tanzania sio maskini bali umaskini wa watanzania unatokana na mgawanyo wa raslimali usio wa haki. Keki ya taifa wanakula wateule wachache na kuwaachia wanachi makombo. Tudadili na tutafute mikakati ya kuwezesha watanzania wote kufaidi keki ya taifa na matunda ya uhuru kwa haki.

Anthony Rwegasira (Community Empowerment Foundation (COEF))
July 20, 2011 at 8:59 PM EAT (edited March 26, 2012 at 8:06 AM EAT)

ARDHI, UWEKEZAJI NA HATMA YA MTANZANIA

Jamani kila kukicha utasikia mwekezaji kapewa maelfu ya ekari za ardhi kwa ajili ya uwekezaji. Ardhi inayotwaliwa ni ile yenye makazi ya watanzania wanyonge. Hali ya kuuza nchi kwa vipande ikiendelea, hatima ya watanzania itakuwaje? Tujadili

 

[message deleted]
Angel (Kagera)
August 15, 2011 at 9:13 PM EAT (edited March 26, 2012 at 8:06 AM EAT)

Watanzania laleni. Mtajiju


Add New Message (Hide)

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.