Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

     MALENGO YA CHAVITA

 

Kama wanajamii, viziwi wanayo haki ya kuchangamana na watu wengine na kushirikishwa  kikamilifu katika shughuli za jamii. Hii ni haki ya msingi ya binadamu. CHAVITA itahakikisha  hili kwa:

 

  • Kuhamasisha matawi ya CHAVITA na jamii ya Viziwi popote walipo hapaTanzania, jamii ya watanzania, taasisi na serikali kuhusu haki za Viziwi.
  • Kupigania usawa katika fursa za elimu, huduma za jamii na nyanja zote za maisha ya binadamu.
  • Kupigania kutambulika kisheria kwa Lugha ya Alama yaTanzania.
  • Kujenga mwamko na kukuza matumizi ya Lugha ya Alama kwa matawi ya CHAVITA, jamii ya Viziwi nchini, na kwa jamii ya watanzania kwa ujumla.
  • Kuhakikisha shughuli za maendeleo ya jamii na ki-uchumi kwa matawi ya CHAVITA na jamii ya Viziwi nchini zinaboreshwa.
  • Kuhakikisha matawi ya CHAVITA na jamii ya Viziwi nchini wanapata uwakilishi katika ngazi zote za uongozi.
  • Kufanya na kuendeleza utafiti kuhusu masuala yanayowahusu Viziwi
  • Kupambana na Virusi vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI pamoja na majanga mengine yanayowakabili Viziwi.

 

Latest Updates
CHAMA CHA VIZIWI TANZANIA CHAVITA-TAWI LA MKOA WA DODOMA added a News update.
chavita dom haikuwa nyuma katika shughuli zake katika kusaidia watoto wenye ulemavu viziwi kama pichani ni watoto viziwi wa shule ya msingi kigwe wakifurahia jambo.
December 15, 2012
CHAMA CHA VIZIWI TANZANIA CHAVITA-TAWI LA MKOA WA DODOMA added 2 News updates.
pichani washiriki wa mafunzo yaliyoendeshwa na chavita dodoma kwa ufadhili wa fcs. ni wanachuo na wazazi wa viziwi na viziwi wenyewe yalifanyika ukumbi wa cct dodoma mjin.
July 14, 2012
CHAMA CHA VIZIWI TANZANIA CHAVITA-TAWI LA MKOA WA DODOMA added 2 News updates.
pichani ni kwaya ya wanafunzi viziwi wa shule ya viziwi kigwe wakiwa katika kanisa la viziwi kigwe wilayan bahi mkoa wa dodoma.
May 31, 2012
CHAMA CHA VIZIWI TANZANIA CHAVITA-TAWI LA MKOA WA DODOMA created a Projects page.
Chavita inajiandaa kuweka ripoti ya miradi hivi karibu..
February 9, 2012
CHAMA CHA VIZIWI TANZANIA CHAVITA-TAWI LA MKOA WA DODOMA created a Team page.
CHAVITA Makao makuu na CHAVITA wilaya ya Dodoma mjini
February 9, 2012
CHAMA CHA VIZIWI TANZANIA CHAVITA-TAWI LA MKOA WA DODOMA added FCS to its list of Partner Organizations.
February 9, 2012
Sectors
Location
DODOMA, Dodoma, Tanzania
See nearby organizations