Log in
ASASI YA MAENDELEO USTAWI NA AFYA

ASASI YA MAENDELEO USTAWI NA AFYA

Masasi, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations
AMUA katika kipindi cha Oktoba- Disemba itaandaa kongamano la kuzungumzia visababishi na madhara ya mimba na ndoa za utotoni kwenye kata za Nanjota, Lipumburu na Lupaso wilayani Masasi. Lengo likiwa ni kuibua mawazo na changamoto kutoka kwa jamii. Washiriki watatoka kwenye maeneo husika.
Asasi ya Amua imeandaa mafunzo ya siku 30 kwa walimu wa kisomo cha watu wazima(wazee). Lengo ni kupata waalimu watakaowafundisha wazee Kusoma, kuandika na kuhesabu. Mafunzo hayo yataendeshwa na wakufunzi toka shirika la Amua lenyewe wakiongozwa na Mratibu wa mafunzo ni Bi Kate Mwembere na yataanza tarehe 15 Julai 2017. Wahitaji wa mafunzo hayo wameanza kuandikishwa.
Baada ya kimya cha muda mrefu asasi ya AMUA imerejea tena katika utoaji wa taarifa kwa umma kwa kupitia ukurasa huu. Ni matarajio yetu kuwa jamii ya wapenda maendeleo wataendelea kuungana nasi katika kuibua hoja na mijadala mbalimbali yenye kuleta maendeleo na kukuza ustawi wa jamii zetu.