Log in
Temeke Youth Development Network

Temeke Youth Development Network

Temeke/Chang'ombe, Tanzania

TEYODEN yaendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana.

Mtandao wa vijana upo katika harakati za kuinua uelewa wa vijana katika masuala ya  ujasiriamali kwa vijana ambao wapo tayari kubadilisha maisha yao kutokana na kubadili mitazamo yao kutoka kukaa tu vijiweni au kumaliza shule/chuo na kulandalanda mtaani bila kufanya chochote.Takwimu zinazotokana na sensa ya watu ya mwaka 2012 inaonyesha vijana ni asilimia karibu 60 ya watu wote nchini na vilevile kwa mujibu wa sera ya maendeleo ya vijana Tanzania vijana ni asilimia 68 ya nguvu kazi ya taifa lakini vijana ndio wahanga wakuu katika upatikanaji wa ajira nchini.Hivyo mbadala pekee kwa ajira umebaki kuwa ujasiriamali na uzalishaji mali. 

Lengo letu ni angalau kuwafanya vijana wabadili mitazamo kutoka mawazo ya kuajiliwa au kukaa tu vijiweni na kuanza kufikiria kijasiriamali kwa kubadili mawazo yao ya kawaida kuwa mawazo ya kijasiriamali na miradi ya kiuchumi.

Mafunzo yanategemewa kuwa ya siku 5 yameanza tarehe 8 na yataisha tarehe 12 mwezi huu wa sita mwaka 2016.Baada ya mafunzo haya kuisha tunategemea kuendeleza kwa vijana wengine mpaka tufikie idadi ya vijana 100.Vijana wanakaribishwa kutoka nyanya na umri tofauti kuja kupata mafunzo.

 

June 9, 2016
« Previous Next »

Comments (1)

Mario Kisonga (Temeke) said:
Nawakubali TEYODEN mnafanya vyema.
June 9, 2016

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.