Injira
Temeke Youth Development Network

Temeke Youth Development Network

Temeke/Chang'ombe, Tanzania

Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Icyongereza. Edit translations

MABADILIKO KWA WALENGWA WA MRADI WA MABINTI WALIO PEMBEZONI YAENDELEA KUONEKANA.

“Mafunzo ya stadi za maisha,elimu ya ujasiriamali na uwezeshaji wa mtaji wa kuanzia biashara umenifanya nibadilishe mtazamo na matendo yangu kuelekea kwenye hatua za mabadiliko”anasema Nuru Matimbwa,Mnufaika wa mradi wa Mabinti walio na watoto chini ya umri wa miaka 20.

Nuru Matimbwa ambaye kwa sasa anasaidia wasichana wengine takribani 10 katika ofisi yake kujifunza masuala ya ushonaji wa nguo za kina mama na biashara ya kuuza khanga na batiki, alikuwa katika kipindi kigumu baada ya kuzalishwa na kutekelekezwa na mchumba wake aliyemdanganya kuwa atamuhudumia kwa kila kitu.Baada ya mafunzo na uwezeshaji alipata matumaini mapya na kuendelea.Ukifika katika ofisi yake utawakuta wasichana takribani 4 wakiwa katika mashine zake, wakibadilishana kwa shifti akiwafundisha ujuzi huo wa kushona ili nao waweze kujiajili.

Nuru anawashauri vijana wengine wakike kuwa wasidanganywe na wavulana na kujikuta wanaharibu mtiririko wa maisha yao kwa kupata watoto kabla ya muda muafaka.Mtoto ni jambo la msingi na la lazima lakini ni vyema kuzaa wakati umeshajiandaa kwaajili ya makuzi na ustawi wa mtoto huyo.Anawashauri wakumbuke kuwa malezi ya mtoto kwa asilimia zaidi ya 70 yanamtegemea mama ambaye nae pia ni mtoto hivyo sio rahisi kulea watoto katika umri mdogo

.”nawashauri msome jamani,kwa ambao tayari mmeshafanya makosa msikate tamaa” anamalizia Nuru

Mnufaika huyu wa awamu ya pili ya mradi kutoka kata ya Azimio ameweza kupata nafasi kadhaa za mafunzo na safari nje ya Dar-es-salaam ili aweze kukuza uelewa wake zaidi.

Mradi wa mabinti walio pembezoni ni hatua ya mwanzo katika kuwasaidia mabinti ambao wamepata mimba katika umri mdogo na wanaoishi katika mazingira hatarishi.Mradi huu unatekelezwa katika kata 3 za Azimio, Mtoni na Kibada na umewezesha wasichana kujitambua na kuchukua hatua mpya katika kujitegemea na kusaidia watoto wao.

      

3 Nyakanga, 2014
« Inyuma Ahakurikira »

Ibitekerezo (1)

farida (sinza) bavuzeko
nuru kaya mwendo dada mungu atakusaidia
26 Nyakanga, 2014

Tanga igitekerezo

Izina ryawe:
Aho uherereye
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.