Log in
Temeke Youth Development Network

Temeke Youth Development Network

Temeke/Chang'ombe, Tanzania

VIJANA MANISPAA YA TEMEKE SASA KAENI MKAO WA KULA.

TEYODEN katika hatua ya kutia moyo wamepata nafasi ya kuwa na mwalimu wa ujasiriamali aliyewezeshwa na ILO kupatiwa mafunzo ya anzisha na kuza wazo la biashara.Start and improve your business idea (SIYB).

Baada ya mafunzo haya,moja ya kazi za mwezeshaji huyu ni kuhakikisha kuwa vijana na wafanyabishara wengine wanakuwa wafanyabiashara zenye kuleta tija na kuondoa mazoea ya kufanya biashara kienyeji.

TEYODEN inategemea kutengeneza mpango kabambe wa kuwafanya vijana ambao hawana biashara lakini wanamawazomazuri ya biashara kuyaweka katika mpango maalumu wa kuyatekeleza,kuyatafutia mitaji na kuyatekeleza kwa vitendo.Lakini pia wale ambao tayari wanabiashara kuboresha biashara hizo ili zitoe tija na zizalishe ajira kwa vijana wengine. 

Wakati ukiwa tayari hapo baadae mwishoni mwa mwezi wa Mei programu hii itaanza na kunufaisha vijana.Wazo ni kufikia angalau vijana 600 wa kata 30 za manispaa ya Temeke.

May 17, 2014
« Previous Next »

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.