Envaya

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Jumatatu 6 July 2015

 ASASI ZA KIRAIA ZAITAKA SERIKALI KUSITISHA KURIDHIA MKATABA/ITIFAKI YA ARIPO – AMBAO UNATISHIA UHURU WA NCHI NA HAKI ZA WAKULIMA

Asasi za kiraia zipatazo 20 zinazounda mtandao wa bioanuai Tanzania unaitaka serikali kusitisha/kusimamisha kwa muda kuridhia itifaki yenye utata ya ARIPO iliyopangwa kutiwa saini katika mkutano wa mawaziri wa nchi wanachama Jumanne, ya tarehe 7.

Mataifa 19 ya Afrika, ambao ni wanachama wa shirika la Haki miliki za kitaaluma la Kanda ya Afrika (the African Regional Intellectual Property Organization (ARIPO), wanakutana Arusha kukubaliana kuhusu mkataba/itifaki ya kimataifa ya mbegu ambayo itachukua mamlaka ya nchi kuratibu wagunduzi wa mbegu (Plant Breeders), na kupiga marufuku haki ya wakulima kuhifadhi, kushirikiana na kubadilishana mbegu.

Mtandao wa TABIO unaguswa na itifaki hii kwa kuwa inazima uhuru wa nchi kwa kuweka sheria ya ARIPO. Kwa mujibu wa Itifaki ya ARIPO, haki za wagunduzi wa mbegu zitatolewa na ofisi ya ARIPO kwa wagunduzi husika. Hata hivyo, nchi husika hazitaweza kuingilia maamuzi ya ARIPO kwa namna yoyote ile. Kitendo hiki kitawabana wakulima wetu ambao wanategemea sana mbegu za asili. Itifaki inatishia usalama na uhakika wa chakula kwa kuwa asilimia 75 ya wakulima wa Tanzania hutegemea mbegu wanazozihifadhi wao wenyewe kwa matumizi ya kilimo. Mfumo wa kibiashara wa mbegu unalenga tu mazao machache ya kibiashara na kudhoofisha bioanuai tajiri na muhimu  inayolindwa na wakulima wadogo. Jamii ya wakulima wa Tanzania haiwezi kukubali sera na sheria ambazo hazizingatii na kushirikisha wakulima wadogo au wawakilishi wao.

Ongezeko la kutilia mkazo mbegu za kibiashara limeshindwa kutatua matatizo ya msingi ya mkulima. Badala ya kukandamiza na kuwahukumu au kuwapiga marufuku wakulima wadogo kuhifadhi na kutumia mbegu zao za asili, serikali husika na hasa Tanzania inatakiwa kuwashughulikia wale wote wanaoingiza mbegu feki hapa nchini ambazo zinawapotezea wakulima fedha na muda wao na hatimaye kushindwa kulisha familia zao na taifa kwa ujumla. Zaidi ya asilimia 75 ya mbegu huzalishwa na wakulima wadogo. Mfumo wa mbegu za kibiashara unatakiwa uishi pamoja na ule wa mbegu za asili zinazomilikiwa na mkulima na siyo kuuondoa huu wa mbegu za asili.

Kama wanachama wa Mtandao wa Uhuru wa chakula Afrika (Alliance for Food Sovereignty in Africa), TABIO inaunga mkono kwa nguvu zote msimamo wa AFSA wa kuzitaka nchi za Afrika kuikataa itifaki hiyo.

Hivyo, TABIO inaitaka serikali ya Tanzania kusimamisha mchakato huu wa haraka wa kuiridhia itifaki ya ARIPO. Maamuzi haya muhimi ni vyema yakachalaweshwa mpaka ushauri wa uwazi na shirikishi ufanywe kwa kushirikisha wakulima na asasi za kiraia. Uhuru wa sheria za Tanzania na haki za mamilioni ya wakulima wake haviwezi kuwekwa pembeni kwa ajili ya maslahi ya kibiashara ya watafiti wa mbegu.

Wasiliana na

Abdallah Ramadhani Mkindi, TABIO Coordinator.

Email: tabiosecretariat@gmail.com, Tel: +255 784 311 179

 

July 6, 2015
« Previous Next »

Comments (1)

Shawn Pablo (USA) said:
I'm a professional in all kinds of hacking services, which leads me into giving out a blank ATM card to all individuals & serious minded people only. I hack, clone ATM cards worth's the total sum of $500,000.00 United States Dollars, with this card you can withdraw the sum of $3500 as daily limit till you cash out the sum total said sum & this cards has been cloned & hacked in the manner that you'll never be caught not detected during usage. For more info, kindly email us: fastatmhackers@gmail.com OR Call/WhatsApp: +16626183756

February 15, 2019

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.