Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

MADHUMUNI

 Shirika litakuwa na madhumuni yafuatayo: -

(a)    Kufanya tafiti mbalimbali zinazohusu maendeleo ya jamii na kuziandika katika vyombo mbalimbali vya habari;

(b)   Kuijengea uwezo jamii iweze kuzuia, kukabiliana na kuondoa changamoto zote wanazokutana katika kufikia maisha bora na mazuri;

(c)    Kurekodi, kutunza na kusambaza taarifa na kumbukumbu mbalimbali zinazohusiana na maendeleo ya wananchi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania;

(d)   Kuongeza, kuimarisha, kuratibu na kulinda ushiriki wa wananchi wa Tanzania katika shughuli mbalimbali zinazowahusu ndani na nje ya ya nchi;

(e)    Kusaidia na kuhamasisha wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kuwasaidia wananchi wenye uhitaji wakati wa hali ya kawaida na wakati wa majanga;

(f)    Kuanzisha na kuendesha benki ya takwimu za maendeleo;

(g)    Kubaini na kuvitangaza vivutio vya uwekezaji, na kuelimisha na kuhamasisha jamii kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji na kuvutia wawekezaji wa ndani na nje;

(h)   Kuhakikisha Tanzania inatawaliwa kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizowekwa na mamlaka  husika;

(i)     Kuratibu ubadilishanaji wa taarifa na ujuzi kwa maendeleo kati ya wananchi wa Tanzania na watu wengine walio ndani na nje ya nchi.

MRADI AMBAO TUMEKWISHAFANYA KUWAJENGEA UWEZO WANACHAMA NA VIONGOZI WA SHIRIKA

 

                Telegraphic Address, SHIMMAKUTA P.O.BOX 20, MTWARA, TANZANIA (EA)

                             Tel: +255 0713 609255, 0652 200630, 0784 573340 E-mail:shimmakuta@gmail.com 

                       SHIRIKA LA MAENDELEO, MAWASILIANO NA KUONDOA UMASKINI TANZANIA     

 

 

10/04/2011

Kumb. Na. SHIMM/NGO/02/02

 

 

MKURUGENZI MTENDAJI,

THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY,

S.L.P 7192

DAR ES SALAAM

 

 

YAH: TAARIFA YA UTEKELEZAJI MRADI WA KUWAJENGEA UWEZO WANACHAMA, VIONGOZI NA WATENDAJI WA SHIRIKA LA SHIMMAKUTA,

MWAKA 2011

 

Husika na somo la barua hii,

 

SHIMMAKUTA kwa heshima kubwa kama mashirika mengine yasiyo ya kiserikali inajishughulisha na kupambana na umasikini uliokithiri katika jamii hii, kwa kuzingatia hilo iliona ni muhimu kuanza na viongozi katika safari hiyo, ndiyo maana ikawasilisha maombi ya ruzuku ya shilingi milioni sita laki tisa hamsini na mbili elfu na mia nane tu, kwa mara ya kwanza kutoka katika taasisi yako ya The foundation for civil society na kufanikiwa kuzipata.

 

Shirika liliamua kuanza na viongozi na wanachama ni kutokana na ukweli kwamba kulikuwa na kasoro ambazo bila ya kuziondoa kwanza shirika lisingeweza kujiendesha, Kwahiyo viongozi na wanachama wakakaa pamoja na kuibua mradi wa kuijengea asasi uwezo wa kujiendesha.

 

Na kamati ikapendekeza kuomba ruzuku kutoka The foundation for civil society na kupata ndogo ya miezi mitatu ya kuwajengea uwezo wanachama na viongozi wa shirika ili mambo yawe sawa.

 

Hivyo basi SHIMMAKUTA ilipokea kiasi hicho hapo juu cha ruzuku na kutekeleza mradi tajwa kwa muda wa miezi mitatu na mabadiliko yaliyokusudiwa yameonekana, na tunategemea baada ya kupokea taarifa hii utaungana nasi kukubali kuwa matokeo yamefikiwa.

 

Natanguliza shukrani kwa kuipokea taarifa yetu hii,

 

 

Godwin.D. Msalichuma,

 

MRATIBU

 

SHIRIKA LA MAENDELEO, MAWASILIANO NA KUONDOA UMASIKINI TANZANIA

 

(SHIMMAKUTA)

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

TAARIFA YA UTEKELEZAJI YA RUZUKU

INAYOWASILISHWA THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY APRILI 2011

KWA AJILI YA KUONYESHA KUTEKELEZWA KWA MRADI WA

KUWAJENGEA UWEZO WANACHAMA, VIONGOZI NA WATENDAJI WA SHIMMAKUTA

MWAKA 2011

 

 

 

 

 

 

Imetayarishwa na:

SHIMMAKUTA

P.O. Box 20,

Mtwara

Tanzania

 

Cell: +255 023 2333757,Fax +255 023 2333757

E-mail: shimmakuta@gmail.com

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

                                                                                                                             YALIYOMO

 

 

 

 

 

 

Dibaji……………………………………………………………………………………….. 1

 

 

 

Kiwiliwili cha taarifa………………………………………………………………………. 2

 

 

 

Utangulizi…………………………………………………………………………………… 2.1

 

 

 

Yaliyojiri wakati wa utekelezaji wa mradi……………………………………………….. 2.2

 

 

 

Majumuisho………………………………………………………………………………… 2.3

 

 

 

Mapendekezo……………………………………………………………………………….. 2.4

 

 

 

Kumbukumbu rejea………………………………………………………………………… 2.5

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

                                                                                                                                               1. DIBAJI

 

 

 

 

 

 

 

 

Kuundwa kwa The foundation for civil society Tanzania na kufanya wafadhili wa nje na ndani kupata sehemu ya kupitishia ruzuku ili kusaidia shughuli za maendeleo nchini kwa kiasi kikubwa asasi nyingi hapa nchini ndogo na kubwa zimekuwa zikipata ufadhili wa kufadhili shughuli za kimaendeleo zinazogusa jamii kutoka ngazi ya vijiji mpaka ngazi ya Taifa.

 

SHIMMAKUTA ni miongoni mwa asasi ambayo imeweza kunufaika na ufadhili wa ruzuku ndogo ya kutekeleza mradi wa kuijengea uwezo haswa viongozi na wanachama kwa malengo ya kuifanya iweze kujiongoza yenyewe bila matatizo ili kuondoa umaskini miongoni mwa wananchi wa Tanzania.

 

Kuwepo kwa The foundation for civil society na utendaji wake mzuri kumeleta faraja kwa wananchi wengi kwani kwasasa ufadhili umekuwepo kwa awamu tatu kwa Mwaka hivyo kufanya asasi nyingi kupokea ruzuku na mafunzo ya kusimamia miradi ya kijamii.

 

Pia FCS imeimarisha utawala bora na uwajibikaji miongoni mwa asasi mbalimbali hapa nchini kwani wamekuwa wakitoa mafunzo ambayo yanaziwezesha asasi hizo zinazopopokea ruzuku kutoka katika shirika hilo zinakuwa na uelewa wa jinsi gani ya kutumia vizuri rasimali fedha na watu kwa ujumla.

 

Katika taarifa hii tutaona jinsi shirika la SHIMMAKUTA lilivyonufaika na mradi wa miezi mitatu wa kujijengea uwezo ambapo viongozi na wanachama ndiyo waliyokuwa walengwa wa ufadhili huu.

 

Ufadhili umeiwezesha asasi kuendesha mafunzo kwa viongozi na wanachama kuweza kuitambua katiba na miundo ya ndani na nje na kupata uelewa wa kuendesha shirika kwa ujumla.

 

Tuwe sote tuangalie jinsi wanufaika walivyoyapata matokeo yaliyokusudiwa katika mradi huu.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

2 KIWILIWILI CHA TAARIFA

 

Shirika liliamua kuanza na viongozi na wanachama ni kutokana na ukweli kwamba kulikuwa na kasoro zifuatazo kiutendaji ndani na nje,

 

      Kutokufanyika vikao na mikutano ya shirika kwa mujibu wa katiba

      Maombi ya ruzuku toka katika shirika kwenda kwa wafadhili kutokukubalika

      Kutofanyika ufuatiliaji, tathmini na uandishi wa taarifa za shughuli zinazotekelezwa na shirika

      Ujuzi mdogo wa kuendesha shirika lisilo la kiserikali miongoni mwa wanachama, viongozi na watendaji wa shirika

      Wanachama, viongozi na watendaji wa shirika kutokuwa na ujuzi wa kutosha wa uongozi na utawala wa shirika lisilo la kiserikali

      Wanachama, viongozi na watendaji wa shirika kutokuwa na ujuzi na mbinu za kubuni miradi na kuandika michanganuo ya miradi (kuchangisha rasilimali)

      Wanachama, viongozi na watendaji wa shirika kutokuwa na ujuzi wa kutosha wa kufuatilia, kutathmini na kutoa taarifa za shughuli zinazotekelezwa na shirika lao.

      Baada ya kuona kasoro hizo wajumbe na viongozi wakaamua kuibua mradi wa kuijengea uwezo asasi na kupata ufadhli kutoka FCS,

      Mafunzo yalifanyika kwa muda wa siku saba ya kuwajengea uwezo wanachama na viongozi wa shirika lisilokuwa la kiserikali

 

Ilifanyika pia ziara ya mafunzo kutembelea Msoapo na Mdamnet,

 

Changamoto zilizojitokeza ni:

      Ugumu wa kupata wanachama ambao wanaoweza kujitolea kuliko kuangalia faida kwanza,

      Ushiriki wa serikali na watoa maamuzi wengine katika shughuli za asasi ndogondogo si wakuridhisha, wanaangalia asasi kubwa na zinazotoa posho na jamii pia wamekuwa wagumu mpaka wasikie kuna posho ndiyo wanajitokeza,

 

 

2.1 UTANGULIZI

 

 

Shirika liliamua kuanza na viongozi na wanachama ni kutokana na ukweli kwamba kulikuwa na kasoro zifuatazo kiutendaji ndani na nje,

 

Kutokufanyika vikao na mikutano ya shirika la kwa mujibu wa katiba,

 

Maombi ya ruzuku toka katika shirika kwenda kwa wafadhili kutokukubalika,

 

Kutofanyika ufuatiliaji, tathmini na uandishi wa taarifa za shughuli zinazotekelezwa na shirika,

 

Ujuzi mdogo wa kuendesha shirika lisilo la kiserikali miongoni mwa wanachama, viongozi na watendaji wa shirika,

 

Wanachama, viongozi na watendaji wa shirika kutokuwa na ujuzi wa kutosha wa uongozi na utawala wa shirika lisilo la kiserikali,

 

Wanachama, viongozi na watendaji wa shirika kutokuwa na ujuzi na mbinu za kubuni miradi na kuandika michanganuo ya miradi (kuchangisha rasilimali),

 

Wanachama, viongozi na watendaji wa shirika kutokuwa na ujuzi wa kutosha wa kufuatilia, kutathmini na kutoa taarifa za shughuli zinazotekelezwa na shirika lao.

 

Na baada ya kufanyika mradi wa kuwajengea uwezo wanachama na viongozi wa mafunzo ya siku saba ya kuijua katiba vizuri na jinsi ya kuendesha shirika kwa ujuzi unaotakiwa hivyo mambo yakawa kama ifuatavyo:

 

v  Vikao na mikutano ya shirika sasa inafanyika kwa mujibu wa Katiba na taratibu zinazotakiwa,

v  Dalili za kukubaliwa kwa maombi ya ruzuku kwa wafadhili yanayotoka katika shirika zinaonekana,

v  Kufanyika kwa ufuatiliaji, tathmini na uandishi wa taarifa za shughuli zinazotekelezwa na shirika,

v  Kuongezeka ujuzi na mbinu za kuendesha shirika lisilo la kiserikali kwa wanachama, viongozi na watendaji wa SHIMAKUTA kutoka 35% ya sasa hadi 55% ilipofika Aprili 2011,

v  Wanachama, viongozi na watendaji wa shirika wamekuwa na ujuzi wa kutosha wa uongozi na utawala wa shirika lisilo la kiserikali,

v  Wanachama, viongozi na watendaji wa shirika wamekuwa na ujuzi na mbinu za kubuni miradi na kuandika michanganuo ya miradi (kuchangisha rasilimali),

v  Wanachama, viongozi na watendaji wa shirika wamekuwa na ujuzi wa kufuatilia, kutathmini na kutoa taarifa shughuli zinazotekelezwa na shirika lao.

 

2.2 YALIYOJIRI WAKATI WA UTEKELEZAJI

 

 

Mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kuendesha shirika kati ya viongozi na wanachama kwa muda wa siku saba ambapo kulikuwapo na ziara ya mafunzo iliyofanyika kuitembelea asasi ya MSOAPO kuangalia ni jinsi gani walianza kufanya kazi na wanakabiliana na changamoto za kupambana na umaskini.

 

Changamoto kubwa tuliyokutana nayo katika utekelezaji wa mradi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wanachama na viongozi ni kwamba baadhi yao kuwa na mawazo ya kulipwa ndiyo waweze kushiriki katika kundesha shirika lao.

 

Washiriki wa mafunzo walikuwa wakishirikiana vizuri na wawezeshaji katika mada mbalimbali pamoja na kuchangia kwa mawazo yao ni jinsi gani tunaweza kuboresha mambo mbalimbali ndani ya shirika lao ukizingatia wengi walianza kuona kuwa ushiriki wa pamoja na kujitolea katika jaimii kuna manufaa makubwa katika kuleta maendeleo ya Taifa.

 

2.3 MAJUMUISHO

 

Kwa ujumla mradi ulifanyika kwa ushirikiano mzuri na mafanikio yalionekana waziwazi kuanzia mwanzo wa mradi baada ya kuipitia katiba na vipengele vyake, washiriki walianza kutambua kuwa kumbe wanapaswa kujitolea kwanza ndipo mambo yanaweza kwenda kuliko kuanza kutaka kuona rasimali fedha kwanza kabla ya kujitolea.

 

Kulingana na uwezo wa wawezeshaji siku saba za mradi wa mafunzo ulitosha sana kuona kuwa mabadiloko tarajiwa yanaonekana kwani washiriki walianza kutoa mapendekezo ya jinsi gani ya kushirikiana kwa kujitolea kama wakiwa rasilimali watu ili kuvutia ile ya fedha ambayo tuliweza kupata kutoka FCS.

 

Na waliweza kuwapongeza FCS kwa kutoa ruzuku kwani wameweza kuona faida ya rasilimali fedha ukijumlisha na rasilimali watu jinsi inavyoweza kuleta maendeleo ya kweli.

 

 

2.4 MAPENDEKEZO

 

 

Mapendekezo tuliyonayo kwa mfadhili wetu kuwa maombi ya ruzuku yanapowafikia kuyashughulikia kwa wakati kwani yakicheleweshwa vitu hupanda bei na kufanya bajeti kutotosha kukidhi haja ya matumizi katika shughuli za mradi husika.

 

2.5 KUMBUKUMBU REJEA

 

 

 

 

Washiriki wa mafunzo ya kujengea uwezo asasi ya SHIMMAKUTA

 

 

 

Baadhi ya washiriki wakiwa katika kazi za vikundi

 

 

 

 

 

Mweka hazina wa Msoapo Bw. Mstapha Kwiyunga akiongea na viongozi na wanachama wa SHIMMAKUTA hawapo pichani, wakiwa katika ziara ya mafunzo katika Ofisi za Msoapo mjini Mtwara.

 

 

 

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kujengewa uwezo juu ya kuendesha shirika la SHIMMAKUTA wakimsikiliza mweka hazina wa Msoapo Bw. Kwiyunga hayupo pichani, akieleza walikotoka mpaka walipo katika kuendesha shirika lao lisilo la kiserikali.