Fungua
SHIRIKA LA MAENDELEO, MAWASILIANO NA KUONDOA UMASKINI TANZANIA

SHIRIKA LA MAENDELEO, MAWASILIANO NA KUONDOA UMASKINI TANZANIA

MTWARA MJINI, Tanzania

Washiriki wa mafunzo wakiwa katika kazi za vikundi

Mwezeshaji wa mafunzo ya kujenga uwezo kuhusu utetezi wa masuala ya jinsia na ukimwi kwa Azaki Bw.Baltazari Komba akiwa katika kipindi ukumbini hapo.

MTANDAO WA MASHIRIKA YASIYOKUWA YA KISERIKALI KATIKA WILAYA YA MTWARA wameendesha mafunzo ya siku mbili juu ya kuwajengea uwezokuhusu utetezi wa masuala ya jinsia na ukimwi kwa Azaki wanachama juzi na jana katika manispaa ya Mtwara yaliyofadhiliwa na GIZWashiriki wa mafunzo ya kujenga uwezo kuhusu utetezi wa masuala ya jinsia na ukimwi kwa Azaki yaliyofadhiliwa na GIZ.

Na Godwin Msalichuma,

Newala, Mtwara

Septemba 29, 2011

JAMII katika Wilaya ya Newala wametakiwa kuanzisha madarasa ya elimu ya watu wazima ili kuondokana na tatizo la ujinga na umaskini uliokothiri haswa kipindi hiki Tanzania inavyoadhimisha miaka hamsini ya uhuru.

Hayo yalisemwa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Bw. Chitwanga Ndembo katika maadhimisho ya juma la elimu ya watu wazima yaliyofanyika kiwilaya katika kijiji cha Mkunya  ambayo yaliandaliwa na asasi isiyokuwa ya kiserikali ya Umoja wa maendeleo ya elimu Newala (NEDA).

“ Wananchi mliyekuja hapa ni mabalozi wa wengine ambao hawakuja ninaagiza kuwa anzisheni madarasa ya elimu ya watu wazima katika maeneo yenu mnayoishi na hiyo ndiyo ujumbe wetu katika kipindi hiki cha maadhimisho ya miaka hamsini ya uhuru wa taifa letu…….anzisheni na hamasisheni watu wajiunge na kunufaika na madarasa hayo” alisema Bw. Ndembo.

Alisema kuwa jamii inapaswa kuelimika zaidi kipindi hiki kwani hata Halmashauri yake imeshajipanga kuanzisha Benki ya maendeleo ya watu wa Newala hivyo basi kunahitajika wananchi angalau walioelimika ili wafungue ankaunti pamoja na kuwa na hisa katika taasisi hiyo ya fedha itakayofunguliwa.

Aidha aliwaomba jamii hiyo kuchangamkia masuala ya elimu ya watu wazima kwani kutawafanya wajue umuhimu wa elimu na kuhamasika kuchangia maendeleo ya elimu ya watoto wao kama vile nyumba za walimu, madarasa na madawati.

“ Mzazi unapoelimika inakusaidia hata wewe mwenyewe kuwa makini katika kuchangia elimu ya watoto ulionao……isitoshe hata masuala ya ukulima wa kisasa wa zao letu kuu la korosho litazingatiwa hivyo kupata mazao bora na kipato cha kutosha kuendeleza afya na elimu ya familia yako” alisema Mwenyekiti huyo.

large.jpg

Baadhi ya washiriki wakiwa katika kazi za vikundi

large.jpg

Washiriki wa mafunzo ya kujengea uwezo asasi ya SHIMMAKUTA

large.jpg

Mweka hazina wa Msoapo Bw. Mstapha Kwiyunga akiongea na viongozi na wanachama wa SHIMMAKUTA hawapo pichani, wakiwa katika ziara ya mafunzo katika Ofisi za Msoapo mjini Mtwara.

large.jpg

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kujengewa uwezo juu ya kuendesha shirika la SHIMMAKUTA wakimsikiliza mweka hazina wa Msoapo Bw. Kwiyunga hayupo pichani, akieleza walikotoka mpaka walipo katika kuendesha shirika lao lisilo la kiserikali.