Wabunge wa kambi ya upinzani wamependekeza posho za vikao vya wabunge zikatwe ili pesa itakayokatwa iwekwe kwenye kasma nyingine za miradiya maendeleo. Makada wa CCM, wabunge na Spika wao hawataki posho hizo ziguswe. Wnasahau yafuatayo:
1. Kulipwa mara mbili kwa kazi ileile ni ufisadi.
2. Kipatao wanachokipata kutokana na posho za vikao hakikatwi kodi, na huu ni ufisadi.
3. Posho wanazopata ni kubwa zaidi kuliko mishahara ya watumishi wengi.
Wanaharakati tutafakari haya mambo tukiweka maanani kwamba Tanzania sio maskini bali umaskini wa watanzania unatokana na mgawanyo wa raslimali usio wa haki. Keki ya taifa wanakula wateule wachache na kuwaachia wanachi makombo. Tudadili na tutafute mikakati ya kuwezesha watanzania wote kufaidi keki ya taifa na matunda ya uhuru kwa haki.