Log in
Christian Education and Development Organization

Christian Education and Development Organization

Nzega District, Tabora Region Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

UWAZI NA UWAJIBIKAJI

Japhet A. Kalegeya (Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi)
July 2, 2011 at 10:49 AM EAT

Uwazi ni njia mojawapo inayoleta mafanikio mema katika shughuli za kimaendeleo. Lakini baadhi ya Halmashari haziko wazi kutoa taarifa mabalimbali za kimaendeleo kwa raia wake. hilli inachelewesha maendeleo katika jamii. raia wengi hawajui mapato na matumizi ya fedha za umma. Tufanyeje ili kupata taarifa za shughuli za kimaendeleo ikiwa ni pamaoja na kushirikishwa katika utengenezaji wa bajeti?

FIKIRI MVUGARO(MWELA THEATRE GROUP) (MTONI MTONGANI TEMEKE DSM)
September 3, 2011 at 7:08 PM EAT (edited March 26, 2012 at 8:06 AM EAT)

Napenda kukushukuru kwa mada yako nzuri mr Jophet A Kalegeya

kutokana na mada yako nzuri ambayo mimi inanihusu moja kwa moja kutokana shughuri zangu ninazofanya

MAJUKUMU YA SERIKALI ZA MITAA.

 

Halmashauri za Manispaa zimeanzishwa chini ya sheria za Mamlaka za Miji (Local Government Urban Authorities Act. 1982).
Majukumu makuu ya Serikali za Mitaa yaliyofafanuliwa na sheria hiyo ni kama ifuatavyo:-

 • Kusimamia na kudumisha amani ulinzi na usalama katika maeneo ya mipaka yake.
 • Kuhamasisha/kuendeleza na kuwapatia huduma bora za kijamii na kiuchumi wananchi walio katika eneo la mipaka ya Halmashauri.
 • Kusimamia sera za maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika maeneo yao.
 • Kuchukua hatua madhubuti za kuhifadhi na kuendeleza mazingira.
 • Kusimamia utawala, fedha, mambo yote ya uendeshaji katika ngazi mbalimbali zilizo ndani ya mamlaka ya Halmashauri ya Manispaa/Jiji.
 • Kusimamia na kuhakikisha demokrasia inadumishwa katika jamii.
 • Kukusanya mapato yatakayowezesha mamlaka ya serikali ya mtaa kuendesha shughuli zake pamoja na kutoa taarifa za matumizi kupitia kamati mbalimbali.
 • Kutoa huduma mbalimbali za kiuchumi na kijamii pamoja na kutekeleza shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
 • Kuzingatia na kutambua masuala mtambuka kama vile Jinsia (accord due recognition to and, promote, gender awareness).
 • 10. Kuendeleza na kusimamia kanuni za biashara, viwanda, kilimo n.k.
 • 11. Kusimamia na kuendeleza huduma za Afya, Elimu, Maji, Utamaduni na masuala ya burudani katika jamii.
 • 12. Kubuni mikakati ya kupambana na umaskini pamoja na mbinu za kusaidia kuboresha maisha ya vijana, wazee, walemavu n.k.

hivyo kutokana na majukumu hayo si hiyari kwa kiongozi   hila tatazo hata baadhi ya viongozi na wananchi awatambui kabisa wajibu wao hivyo basi jukumu la kila mtu amuelimishe kujua majukumu na ya viongozi wake na ajue umuhimu wake wa kushiriki kikamirifu katika serikali ya Mtaa wake na kudai mapato na matumizi nikisema kikamilifu maana kuna watu wao uenda tu lakini awachangii kitu chochote ili tuweze kusimamia vizuri rasilimali za uma na kuwawajibisha wale viongozi wasio kuwa na madli jukumu la viongozi  kuwa na wazi  na uwajibikiji ni letu wananchi kwa mujibu wa katiba ya jamuhuri ya muhungano wa Tanzania ya mwaka 1982 asante sana

 

Christian Education and Development Organization
February 28 at 6:03 AM EAT

@FIKIRI MVUGARO(MWELA THEATRE GROUP) (MTONI MTONGANI TEMEKE DSM): 

Asante Sana Mr.Fikiri Mvungaro kwa mchango wako nzuri wa kutuelimisha kuu ya majukumu ya Halmashauri na uanzishwaji wake.

Add New Message

Invite people to participate