Log in
AFRICAN STUDENTS GOODHEART SOCIETY

AFRICAN STUDENTS GOODHEART SOCIETY

Muheza, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

HAKI ZA WAZEE KWA MATAMKO YA SERA YA TAIFA YA WAZEE, MATAMKO YA KIMATAIFA NA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WAZEE

  • Utangulizi:

Haki ni stahili anayopaswa kupata mtu, kisheria ama kwa kuzaliwa, haki hiii humpa mtu uhuru wa kutenda au kumiliki (Chanzo:kanuni ya Oxford).

Azimio la umoja wa mataifa namba 46 la mwaka 1991 limeweka bayana kuwa wazee wana haki zifuatazo:(i) kuwa huru (ii) kushiriki na kushirikishwa (iii) kutunzwa (iv) kujiendeleza/kukukza utu wake (v) kuheshimiwa [Chanzo: sera ya Taifa ya wazee 2003).

  • Hali ya kiujumla ya wazee:

Kwa mujibu wa sera ya Taifa ya wazee, wazee wanakabiliwa na changamoto nyingi, kama umasikini, magonjwa, kutowekwa katika mipango ya maendeleo, n.k.

Umasikini:

Hii ni tatizo kubwa sana hasa kwa wazee wengi ambao walikuwa katika ajira zisizo katika mfumo rasmi kama wavuvi, wafugaji, wakulima wa mazao. Kwa sababu kundi hili halimo katika mfumo wowote rasmi wa hifadhi ya jamii. Pia wazee wastaafu walio katika mpango wa hifadhi ya jamii wanakumbwa na matatizo yanayotokana na urasimu wa kupata huduma (Chanzo: sera ya Taifa ya wazee, 2003). Mikakati iliyopo sasa haihusishi wazee katika kuondoa umasikini, hii ni kutokana kwa sababu hakuna sheria yeyote inayosimamia utekelezaji wa sera hii.

Magonjwa:

  • Licha ya Serikali kugawa kadi za kuwapatia wazee huduma ya matibabu, changamoto kubwa imejitokeza ya kukosa dawa. Wazee wengi hawana uwezo wa kumudu gharama za ununuzi wa dawa licha ya matibabu kutolewa bure.
  • Ugonjwa wa UKIMWI ambao ni janga kubwa, bado elimu ya kutosha haijatolewa kwa wazee. Wazee hawajumuishwi vya kutosha katika mapambano dhidi ya UKIMWI, licha ya kwamba mzigo wa kuuguza wagonjwa wa UKIMWI majumbani wamebeba wao, pamoja na ulezi wa watoto yatima (sera ya Taifa 2003, uk:10), licha ya sera kutoa ushirikishwaji wa wazee.

Mipango ya maendeleo:

  • Mipango mingi ya maendeleo haiwashirikishi na kujumuisha wazee katika bajeti za halmashauri na ngazi mbalimbali. Hii inatokana na kukosekana kwa uwakilishi katika vyombo vya maamuzi kama Kamati ya maendeleo ya Kata; Baraza la Madiwani na Bunge. Sera ya Taifa ya wazee inasema na kutoa ahadi kwamba: Utawekwa utaratibu utakaowashirikisha wazee katika uandaaji na utekelezaji wa mipango ya maendeleo katika ngazi mbalimbali.

Kutokuwepo kwa mfuko wa wazee:

  • Kutokuwepo na mfuko wa wazee wa kukopa umechangia wazee wengi kushindwa kuanzisha na kuendesha miradi ya maendeleo ambayo wanaimudu. Fursa za kukopeshwa vitendea kazi kama matrekta madogo n.k. ambayo kupitia vijana wa Azaki wangeweza kusaidiwa kulimia mashamba yao. Sera ya Taifa ya wazee ya mwaka 2003 inatoa ahadi kwamba Serikali itaanda mfuko wa wazee (Revolving Loan Fund) kuwawezesha wazee kukopa ili waendeshe miradi yao(Chanzo: Sera ya Taifa ya wazee, 2003).

Kutokuwemo katika hifadhi ya jamii kwa wazee waliostaafu katika ajira zisizo rasmi:

  • Mfumo wa hifadhi ya jamii uliopo unawahudumia wazee waliokuwa wameajiriwa katika sekta rasmi tu. Ikumbukwe ya kwamba wazee wengine pia wamelijenga Taifa, kupitia kodi zao katika shughuli mbalimbali za uzalishaji mali kama kilimo, ufugaji wa mifugo, uvuvi n.k. Kodi zao zilitumika katika kujenga miundo mbinu na n.k.

MAPENDEKEZO:

(i) Kutungwa kwa sheria: Kutokana na kutokuwepo kwa sheria yeyote inayosimamia utekelezwaji wa sera ya wazee, sera hii ya mwaka 2003 imebakia kuwa katika maandishi bila ,kuwepo katika vitendo. Hivyo basi kuwepo kwa sheria kutasaidia utekelezwaji wa sera.

(ii) Halmashauri za wilaya zitenge fedha kupitia mfuko maalumu wa wilaya ili kuwawezesha wazee kupata huduma na pia kuendesha shughuli mbalimbali kupitia katika vikundi.

(iii) Halmashauri kupitia idara ya maendeleo ya jamii na mipango iandae daftari la takwimu kubaini idadi ya wazee.

(iv) Wazee kupata uwakilishi katika vyombo vya maamuzi katika ngazi zote za kata, Halmashauri na Bunge, hii itasaidia kuhakikisha kuwa hawasauliki kuwekwa katika mipango ya maendeleo, aidha kuhakikisha Bajeti inaweka fungu la kuwahudumia wazee.

(v) Halmashauri kutengeneza mbinu/mfumo utakao wawezesha wazee kupata vyote Tiba na Dawa.

(vi) Mgawanyo wa majukumu wa kuwasaidia wazee katika kutekeleza sera ya wazee uzingatiwe na kuwekwa katika vitendo kuanzia serikali kuu hadi ngazi ya familia.

(vi) Baraza ya wazee yatimize wajibu wao wa kuhakikisha kwamba wanasimamia malengo ya uanzishwaji wa Mabaraza hayo ya kudai haki bora ya maisha ya wazee kwa ujumla.Hii ni katika ngazi zote kwa Mabaraza yaliyoundwa tayari, kwani ndiyo sehemu ya kupazi sauti za wazee.

March 20, 2012
« Previous Next »

Comments (4)

joseph henry (lushoto) said:
serikali itimize ahadi yake ya kutoa posho ya kujikimu kwa wazee wote nchini kwani wote ni wastaafu wallitumikia taifa lao tena kwa uaminifu mkubwa,vijana wakiyaona maisha wanayoishi wazee sasa wanaweza hamasika kufanya vitendo vya rushwa na ufisadi kwa kisingizio cha kujianda na maisha ya uzee pia sheria atungwe
July 16, 2012
joseph henry (lushoto) said:
wazee mliopo bungeni wazee wenzenu wa vijijini wanawategemea katika kupigania haki zao ,wazee wamefanya mengi katika kujenga taifa mifano ipo wazi,wamejanga miundombinu kama reli ,mashule,pia amani na mshikamano uliopob ni matunda ya wazee
July 16, 2012
joseph henry (lushoto) said:
Ningekuwa nauwezo ningewakutanisha wazee kutoka kila pande ya Tanzania ili wapate fursa ya kupaza sauti zao kwa pamoja kwani wamebaki kama watoto yatima,sisi vijana hali ya maisha ni ngumu ,kwa wazee wasio na nguvu hali ikoje?
July 16, 2012
joseph henry (lushoto) said:
tTakwimu zinaonesha kuwa idadi ya wazee wataoishi katika mazingira magumu itaongezeka kwa kasi ifikapo mwaka2020 hii ni kutakana na idadi ya vijana wanaoishi kwa kutegemea ajira rasmi inaongezeka wakati urasimishwaji wake ukiwa mdogo
July 16, 2012

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.