Fungua
Jumuiya ya Skuli za Maandalizi za Madrasa Zanzibar

Jumuiya ya Skuli za Maandalizi za Madrasa Zanzibar

MWANAKWEREKWE, Tanzania

FCS Narrative Report

Utangulizi

JUMUIYA YA SKULI ZA MAANDALIZI ZA MADRASA ZANZIBAR
ZPMO
KUJENGEWA UWEZO VIONGOZI NA WANACHAMA WA ASASI YA ZPMO
FCS/RSG/2/10/256
Tarehe: 08 FEBRUARI HADI 07 MACHIKipindi cha Robo mwaka: CHA 1
MOHAMED OTHMAN DAU
P.O.BOX 4105, ZANZIBAR.
EMAIL: mohdothman04@yahoo.com
PHONE: 0777 487 848

Maelezo ya Mradi

Uimarishaji Asasi za Kiraia
MRADI HUU UMELENGA ZAIDI UIMARISHAJI WA ASASI YETU KWA KUSAIDIA KATIKA KUTOA MAFUNZO MBALI MBALI KWA WANACHAMA NA VIONGOZI WA ASASI ILI KUWAJENGEA NA KUWAONGEZEA UWEZO WA KUIONGOZA ASASI KISAYANSI ZAIDI. MAFUNZO YALIYOTOLEWA NI HAYA YAFUATAYO:

1. UENDESHAJI NA USIMAMIZI WA ASASI.
2. USIMAMIZI NA UENDESHAJI WA MIRADI.
3. USIMAMIZI NA UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU ZA FEDHA.
4. KUANDAA MPANGO MKAKATI.

MBALI YA MAFUNZO HAYO MRADI PIA ULIISAIDIA JUMUIYA YA ZPMO KUANDAA MPANGO MKAKATI NA MUONGOZO WA FEDHA WAKE.
MkoaWilayaKataVijijiIdadi ya Wanufaika
Zanzibar WestMAGHARIBIM/KWEREKWEM/KWEREKWE172
 Walengwa wa moja kwa mojaWalengwa wasio wa moja kwa moja
Wanawake8123
Wanaume4919
Jumla13042

Shughuli na Matokeo ya Mradi

VIONGOZI NA WANACHAMA KUWA NA UWELEWA JUU YA USIMAMIZI NA UENDESHAJI WA ASASI,MIRADI,UANDAAJI WA MPANGO MKAKATI, USIMAMIZI, UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU ZA FEDHA NA KUWEZA KUTENGENEZA MPANGO MKAKATI NA MUONGOZO WA FEDHA WA JUMUIYA..
1. KUTOA MAFUNZO YA UENDESHAJI NA USIMAMIZI WA ASASI KWA VIONGOZI NA WANACHAMA WA JUMUIYA 40 KWA SIKU 2.
2. KUTOA MAFUNZO YA USIMAMIZI NA UENDESHAJI WA MRADI KWA VIONGOZI NA WANACHAMA WA JUMUIYA 30 KWA SIKU 2.
3. KUTOA MAFUNZO JUU YA USIMAMIZI NA UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU ZA FEDHA KWA VIONGOZI WA JUMUIYA 20 KWA SIKU 2.
4. KUANDAA MUONGOZO WA FEDHA KWA JUMUIYA YA SKULI ZA MAANDALIZI ZA ZANZIBAR (ZPMO).
5. KUTOA MAFUNZO YA KUANDAA MPANGO MKAKATI WA JUMUIYA KWA VIONGOZI NA WANACHAMA 40 KWA SIKU 2.
6. KUANDAA MPANGO MKAKATI WA JUMUIYA YA SKULI ZA MAANDALIZI ZA ZANZIBAR (ZPMO).
7. UFUATILIAJI NA TATHMINI.
1. MAFUNZO YA UENDESHAJI NA USIMAMIZI YA ASASI KWA VIONGOZI NA WANACHAMA 40 KWA SIKU 2 YALIFANYIKA KATIKA UKUMBI WA ZMRC ZANZIBAR SIKU YA TAREHE 21 NA 22/02/2011 KUANZIA SAA 02:00 ASUBUHI MPAKA SAA 09:30 JIONI. KATIKA MAFUNZO HAYA WASHIRIKI WALIJIFUNZA JUU YA UONGOZI WA ASASI ZA KIRAIA,USIMAMIZI WA ASASI ZA KIRAIA, UANDISHI WA RIPOTI, UANDAAJI WA AJENDA NA KUMBUKUMBU ZA MIKUTANO.

2. MAFUNZO YA USIMAMIZI NA UENDESHAJI WA MIRADI KWA VIONGOZI NA WANACHAMA 30 KWA SIKU 2 PIA YALIFANYIKA KATIKA UKUMBI WA ZMRC ZANZIBAR SIKU YA TAREHE 27-28/02/2011 KUANZIA SAA 02:00 ASUBUHI MPAKA SAA 09:30 JIONI. KATIKA MAFUNZO HAYA WASHIRIKI WALIJIFUZA JUU YA MBINU ZA UANDISHI WA MIRADI, USIMAMIZI WA MIRADI NA UANDAAJI WA BAJETI KWA MIRADI.

3. MAFUNZO JUU YA USIMAMIZI NA UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU ZA FEDHA KWA VIONGOZI WA JUMUIYA 20 KWA SIKU 2 YALIFANYIKA KATIKA UKUMBI WA ZMRC KIPONDA SIKU YA TAREHE 09 NA TAREHE 10/03/2011 KUANZIA SAA 02:00 ASUBUHI HADI SAA 09:30 JIONI. KATIKA MAFUNZO HAYA WASHIRIKI WALIELEWESHWA JUU YA MAANA YA UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU ZA FEDHA,UMUHIMU WA KUWEKA KUMBUKUMBU ZA FEDHA,MATATIZO YA KUTOKUWEKA KUMBUKUMBU ZA FEDHA,NJIA BORA ZA KUTUNZA KUMBUKUMBU ZA FEDHA KWA JUMUIYA KAMA ZPMO,MATUMIZI YA NYARAKA MBALI MBALI ZA UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU ZA FEDHA KAMA VILE RISITI,VOCHA,PETTY CASH VOCHA,LEJA,TARATIBU ZA BENKI,UMUHIMU WA KUWA NA MFUMO MZURI WA MANUNUZI, UTATATIBU BORA WA MANUNUZI,MADHARA YA KUTOFUATA UTARATIBU BORA KATIKA MANUNUZI,MUONGOZO UNAOSIMAMIA TARATIBU NA NYENENDO ZA MANUNUZI HAPA ZANZIBAR, NYARAKA MUHIMU KATIKA MANUNUZI NA HATUA ZA KUFUATA KATIKA MANUNUZI.

4. BAADA YA MAFUNZO, VIONGOZI HAO 20 WALIOPATA MAFUNZO PAMOJA NA MTAALAMU WA MASUALA YA FEDHA WALISHIRIKIANA KUANDAA MUONGOZO WA FEDHA WA JUMUIYA YA SKULI ZA MAANDALIZI ZA MADRASA KUANZIA TAREHE 12 MPAKA 23/03/2011 KATIKA UKUMBI WA ZPMO HAPO MWANAKWEREKWE ZANZIBAR.

5.MAFUNZO JUU YA UANDAAJI WA MPANGO MKAKATI WA JUMUIYA KWA VIONGOZI NA WANACHAMA 40 YALIFANYIKA KATIKA UKUMBI WA ZMRC KIPONDA TAREHE 24 HADI 25/03/2011 KUANZIA SAA 02:00 ASUBUHI MPAKA SAA 09:30 JIONI. KATIKA MAFUNZO HAYA WASHIRIKI WALIWEZA KUJIFUNZA MAMBO MBALIMBALI YANAYOHUSU UANDAAJI WA MPANGO MKAKATI KAMA VILE UCHAMBUZI WA SWOT, MPANGO KAZI, KUTAFUTA VIASHIRIA VYA SHUGHULI NA KUBUNI SHUGHULI.

6. BAADA YA MAFUNZO YA UANDAAJI WA MPANGO MKAKATI WA JUMUIYA WASHIRIKI WA MAFUNZO KWA KUSHIRIKIANA NA MTAALAMU WA MIPANGO WALIKAA PAMOJA KUANDAA MPANGO MKAKATI WA JUMUIYA KUANZIA TAREHE 26/03 HADI 15/4/2011.

7. UFUATILIAJI NA TATHMINI KWA MRADI ULIANZA TAREHE 20 HADI 29/4/2011.KATIKA TATHMINI HII ILIGUNDULIKA KWAMBA MUDA WA MAFUNZO ULIKUWA MDOGO MNO KIASI AMBACHO MABADILIKO KWA BAADHI YA WASHIRIKI KATIKA TAASISSI ZAO MOJA MOJA BADO NI MADOGO HASA KATIKA MASUALA YA FEDHA. HIVYO IKAPENDEKEZWA KWAMBA BADO KUNA HAJA KWA VIONGOZI WA JUMUIYA KUPATIWA MAFUNZO YA USIMAMIZI WA FEDHA ZAIDI NA KISHA VIONGOZI HAWA WATOE MAFUNZO HAYO KWA VIONGOZI WA SKULI MOJA MOJA WANACHAMA. SUALA LA PILI LILILOJITOKEZA BAADA YA TATHMINI NI KJIFUNZA JUU YA HAJA YA WALE WALIOPATA MAFUNZO KUJIFUNZA KWA VITENDO KATIKA UANDISHI WA MIRADI CHINI YA UANGALIZI WA WATAALAMU.
HAKUNA
1. MAFUNZO YA UENDESHAJI NA USIMAMIZI WA ASASI KWA VIONGOZI NA WANACHAMA 40 KWA SIKU 2 YALIGHARIMU KIASI CHA JUMLA YA SHILINGI 1,333,500/-

2.MAFUNZO YA USIMAMIZI NA UENDESHAJI WA MRADI KWA VIONGOZI NA WANACHAMA WA JUMUIYA 30 KWA SIKU 2 YALIGHARIMU KIASI CHA JUMLA YA SHILINGI 1,123,500/-

3.MAFUNZO JUU YA USIMAMIZI NA UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU ZA FEDHA KWA VIONGOZI WA JUMUIYA 20 KWA SIKU 2 YALIGHARIMU KIASI CHA JUMLA YA SHILINGI 913,500/-.


4. KUANDAA MUONGOZO WA FEDHA KWA JUMUIYA YA SKULI ZA MAANDALIZI ZA ZANZIBAR (ZPMO) KULIGHARIMU KIASI CHA JUMLA YA SHILINGI 300,000/-

5.MAFUNZO YA KUANDAA MPANGO MKAKATI WA JUMUIYA KWA VIONGOZI NA WANACHAMA 40 KWA SIKU 2 YALIGHARIMU KIASI CHA JUMLA YA SHILINGI 1,333,500/-

6. KUANDAA MPANGO MKAKATI WA JUMUIYA YA SKULI ZA MAANDALIZI ZA ZANZIBAR (ZPMO) KULIGHARIMU KIASI CHA JUMLA YA SHILINGI 300,000/-

7. UFUATILIAJI NA TATHMINI VILIGHARIMU KIASI CHA JUMLA YA SHILINGI 200,000/-

8. GHARAMA ZA SHUGHULI ZA UTAWALA NA USIMAMIZI WA MRADI NI KIASI CHA JUMLA YA SHILINGI 1,979,000/-

KWA HIVYO GHARAMA ZA MRADI KWA JUMLA NI SHILINGI 7,483,000/-






Mafanikio au Matunda ya Mradi

1. VIONGOZI NA WANACHAMA WA JUMUIYA YA SKULI ZA MAANDALIZI ZA MADRASA KUWA NA UWELEWA JUU YA UENDESHAJI NA USIMAMIZI WA ASASI NA MIRADI.

2. KUWEPO KWA MUONGOZO WA FEDHA NA MPANGO MKAKATI WA JUMUIYA YA SKULI ZA MAANDALIZI ZA MADRASA.
1. JUMUIYA IMEWEZA KUANDAA MIRADI MENGINE NA KUIOMBEA KATIKA TAASISI NYENGINE MBALIMBALI ZA KUSAIDIA KAMA UN HABITAT, USSHF NA UBALOZI WA KANADA.

2. JUMUIYA IMEWEZA KUTUMIA UTARATIBU BORA ZAIDI WA KUTOA NA KUTUNZA FEDHA.

3. JUMUIYA IMEWEZA KUZAA WAZO LA KUIFANYIA MAREKEBISHO KATIBA YAKE ILI KUIBORESHA ZAIDI.

4. JUMUIYA IMEANZA KUFANYA SHUGULI ZAKE KWA KUFUATA MPANGO MKAKATI ULIOTAYARISHWA KUPITIA MRADI HUU.
JUMUIYA IMEKUWA NA DEMOKRASIA ZAIDI KATIKA MAAMUZI MBALI MBALI YANAYOHUSU JUMUIYA. INGAWA KUNA KAMATI NDOGO NDOGO ZILIZOUNDWA NA KUPEWA MAJUKUMU MBALI MBALI LAKINI MAAMUZI YOTE YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU HAYO HUAMULIWA KWA PAMOJA KATIKA JUMUIYA.
HAKUNA

Mambo Mliyojifunza

Maelezo
VIONGOZI WA JUMUIYA HAWAKUWA NA TAALUMA YA KUTOSHA YA UONGOZI NA USIMAMIZI WA JUMUIYA INAYOTAKIWA KABLA.
VIONGOZI NA WANACHAMA WA JUMUIYA YOYOTE WANAPASWA WAWE WABUNIFU ZAIDI NA ZAIDI KATIKA KUJUA MATATIZO YA JAMII WANAYOIFANYIA KAZI NA KUYATAFUTIA UFUMBUZI..
MASUALA YA KUMBUKUMBU NA UTUNZAJI WA FEDHA KATIKA JUMUIYA YANAHITAJI UMAKINI WA ZIADA ILI KUEPUSHA UBADHIRIFU WA FEDHA,MIGOGORO NA KUPARAGANYIKA KWA JUMUIYA HUSIKA.
MASWALA YA FEDHA KATIKA JUMUIYA LAZIMA YAWE NA MUONGOZO MAALUMU AMBAO WATU WATAUFUATA ILI KUWA WAZI ZAIDI NA KUONDOA SHAKA NA MWANYA WOWOTE WA UPOTEVU WA RASILIMALI NA UFISADI..
MPANGO MKAKATI UNAIRAHISISHIA MNO JUMUIYA KUWEZA KUFANYA SHUGHULI ZAKE VYEMA NA KWA MAFANIKIO YANAYOPIMIKA.

Changamoto

ChangamotoNamna mlivyokabiliana nazo
KUCHELEWA KWA FEDHA ZA MRADIKUWASILIANA NA WAHISANI NA KISHA KUPELEKA MBELE UTEKELEZAJI WA MRADI KIDOGO.
MUDA WA MAFUNZO KUWA MDOGO MNO.KUJARIBU KUTAFUTA WAHISANI WENGINE WAKUFADHILI KWA MAFUNZO ZAIDI.
ELIMU NDOGO YA WASHIRIKI WA MRADI.KWENDA NAO KWA MUJIBU WA UELEWA WAO NA KUTUMIA NJIA ZA KUWASHIRIKISHA ZAIDI.

Mahusiano

WadauNamna mlivyoshirikiana nayo
NON-GOVERNMENTAL ORGANISATION CLUSTER.KUTUPATIA MGENI RASMI ILI KUTUFUNGIA MAFUNZO YETU RASMI.
AGAKHAN FOUNDATIONKUTUPATIA MGENI RASMI WA KUTUFUNGULIA MAFUNZO YETU RASMI.
ZANZIBAR MADRASA RESOURCE CENTRE.KWA USHAURI WA HAPA NA PALE KATIKA UTEKELEZAJI WA MRADI NA SHUGHULI ZA JUMUIYA.
.JUMUIYA YA WHITESTAR.KUTUPATIA MKUFUNZI NA USHAURI WA HAPA NA PALE KATIKA UTEKELEZAJI WA MRADI.

Mipango ya Baadae

Shughuli ZilizopangwaMwezi wa 1Mwezi wa 2Mwezi wa 3
MRADI WETU NI WA KIPINDI CHA MIEZI MITATU TU KWA HIVYO HATUTOKUWA NA SHUGHULI NYENGINE ZA KUFANYA ILA TUNATARAJIA KUOMBA RUZUKU ZAIDI KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA MRADI MWENGINE.

Walengwa Waliofikiwa

    Walengwa wa moja kwa mojaWalengwa wasio wa moja kwa moja
Wajane na WaganeWanawakeINAFANYIWA KAZIINAFANYIWA KAZI
WanaumeINAFANYIWA KAZIINAFANYIW KAZI
JumlaINAFANYIWA KAZIINAFANYIWA KAZI
Watu wanaoishi na VVU/UKIMWIWanawakeINAFANYIWA KAZIINAFANYIWA KAZI
WanaumeINAFANYIWA KAZIINAFANYIWA KAZI
JumlaINAFANYIWA KAZIINAFANYIWA KAZI
WazeeWanawake3309
Wanaume1707
Jumla5016
Watoto YatimaWanawakeINAFANYIWA KAZIINAFANYIWA KAZI
WanaumeINAFANYIWA KAZIINAFANYIWA KAZI
JumlaINAFANYIWA KAZIINAFANYIWA KAZI
WatotoWanawakeINAFANYIWA KAZIINAFANYIWA KAZI
WanaumeINAFANYIWA KAZIINAFANYIWA KAZI
JumlaINAFANYIWA KAZIINAFANYIWA KAZI
Watu wenye UlemavuWanawakeINAFANYIWA KAZIINAFANYIWA KAZI
WanaumeINAFANYIWA KAZIINAFANYIWA KAZI
JumlaINAFANYIWA KAZIINAFANYIWA KAZI
VijanaWanawake4814
Wanaume3212
Jumla8026
Watu wengineWanawakeINAFANYIWA KAZIINAFANYIWA KAZI
WanaumeINAFANYIWA KAZIINAFANYIWA KAZI
JumlaINAFANYIWA KAZIINAFANYIWA KAZI
(Hakuna jibu)

Matukio Mliyoyahudhuria

Aina ya TukioLiniMambo uliyojifunzaHatua zilizochukuliwa
MAFUNZO YA USIMAMIZI WA RUZUKU.TAREHE 14 - 15/10/2010KUWEKA KUMBUKUMBU ZA FEDHA NA UANDISHI WA RIPOTI.KUTOA MAELEKEZO KWA VIONGOZI WENGINE WA JUMUIYA NA KUJARIBU KUBORESHA UTARATIBU WA FEDHA KATIKA JUMUIYA.

Viambatanisho

« Iliyotangulia

Ongeza maoni

Jina lako:
Mahali ulipo:
Email yako:
(sio lazima)
Anwani yako ya email haitachapishwa.