Victory Youth Support Organization (VIYOSO) ni shirika la vijana lisilo la kiserikali (NGO) lisilotengeneza faida lililopo ndani ya kata ya Uwanja wa Taifa Mainspaa ya morogoro.
Shirika linafanya miradi mbalimbali kwa vijana yenye lego la kumsaidia kijana wa kitanzania kujitambua na hatimaye kupambana na umasikini kwa njia kujiajili katika shughuli mbalimbali za ujasiliamali.
Pia shirika la VIYOSO linatoa mafunzo mbalimbali kwa vijana kupitia kituo chake cha VICTORY & FAITH TRAINING CENTRE kilichopo manispaa ya Morogoro.
yafuatayo ni baadhi ya matukio yaliyo jitokeza kwenye utekelezaji wa program mbalimbali za shirika la VIYOSO.
vijana wanafunzi wa kozi mbalimbali kutoka katika mradi wa Victory & faith unaoendeshwa na Shirika la viyoso- Morogoro
mkurugenzi wa Shirika la VIYOSO Bwn Freddy Ngatigwa akiwa na mavolontia Jannis na jan kutoka chuo kikuu cha Dusseldorf Nchini ujerumani walipo tembelea mradi wa ICT wa victory & faith morogoro
baadhi ya vijana wakipatiwa mafunzo ya ushonaji kwa lengo la kujiajili kwenye ujasiliamali kutoka katika mradi wa Victory & Faith unaoendeshwa na shirika la VIYOSO
vijana wanafunzi wa uhazili wakipata mafunzo kutoka kwa mwl. Kashimili kwenye kituo cha shirika la viyoso kikitwacho Victory & Faith Training Centre mjini morogoro
Baadhi ya vijana wakiwa kwenye Darasa la uhazili wakipatiwa mafunzo ya Secretarial kutoka kituo cha Victory & faith training Centre moja ya miradi ya Shirika la VIYOSO
Vijana wakipatiwa mafunzo ya ICT kutoka kituo cha viyoso kiitwacho Victory & Faith kilichopo manispaa ya morogoro
vijana wa Viyoso wakipata maelezo ya mambo ya hotel kutoka kwa Mwl. Mkude kituoni Victory & Faith kilichopo manispaa ya Morogoro.