Injira
VITONGOJI ENVIRONMENTAL CONSERVATION ASSOCIATION

VITONGOJI ENVIRONMENTAL CONSERVATION ASSOCIATION

chake-chake, Tanzania

Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

Jumuiya ya Kuhifadhi mazingira Vitongoji (VECA) kwa kipindi hichi inaendesha mradi ushawishi na utetezi wa haki za wanawake na kumiliki ardhi. Mradi huu ni wa miaka 3 na unafadhiliwa Foundation flor Civil Society LTD.

Lengo kuu la mradi ni kuwatetea wanawake ambao wanakosa haki zao za msingi za kumiliki ardhi kutokana na mila na desturi potofu zinazo fanyika katika maeneo mingi ya visiwa vya Zanzibar. Katika hali hii wanaume wanakuwa wanawakosesha wanawake hasa baada ya kuolewa ama wajane kupata rasilimali zao zaidi ardhi, ama endapo wanaipata kunakuwa na kuchelewa katika kurithi, hivyo kufanya wanaume kuhodhi mali zote baada ya kufa wazee.

Hivyo mradi huu unakwenda mbali zaidi kwa kufanya mikutano ya kampeni ya hadhara, maigizo, vipeperushi, T-shirts, midahalo na semina mbali mbali kwa lengo la kumkomboa mwanamke zaidi katika ukanda wa mashariki ya kisiwa cha Pemba ambapo ndiko mradi huu unakotekelezwa

15 Kanama, 2014
« Inyuma

Ibitekerezo (1)

Fatma mohd (Mwanyanya Unguja) bavuzeko
mumekuwa mnafanya vizuri katika kutekeleza miradi na kutoa taarifa mbona muko kimya kipindi hichi ama hamna shughuli munazo tekeleza kwa kipindi hichi?
14 Ukuboza, 2016

Tanga igitekerezo

Izina ryawe:
Aho uherereye
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.