Katika kuhakikisha kuwa mkakati wa kuwajengea uwezo wanawake kiuchumi unafanikiwa kwa kiasi kikubwa, asasi ya Tukutane imeendesha mafunzo ya kutengeneza sabuni ya maji kwa akina mama wa kikundi cha Mwamko kilichopo katika mtaa wa Mseto hapa mkoani Geita, mafunzo hayo ya nadharia na vitendo yametolewa na Afisa mtendaji mkuu ndugu Kim Adiel Segev. Kikundi hicho tayari kimeshatengeneza lita mia moja za sabuni.
June 18, 2013