Fungua

Tafsiri: Kiswahili (sw): Maandiko ya Watumiaji: WIVpmUTa6iCfahlO6T1TErRv:content

« Iliyotangulia   ·   Ifuatayo »
Asili (Kiswahili) Kiswahili
1000777713.jpg


Na neema Nkumbi - Kahama, Shinyanga


Mgombea mwenza wa urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi, ameahidi kuanzisha mashamba darasa 60 kwa ajili ya kufundisha wakulima na wafugaji mbinu bora za kilimo na ufugaji wa ng’ombe wa kisasa endapo chama hicho kitaaminiwa kuendelea kuongoza nchi.


Akihutubia maelfu ya wananchi katika kata ya Kagongwa, Manispaa ya Kahama, Dkt. Nchimbi amesema mashamba darasa hayo yatakuwa chachu ya kuongeza tija kwenye kilimo, kuimarisha mifugo na kuinua kipato cha wananchi hususan vijana na wakulima wadogo.


Mbali na mashamba darasa, alibainisha kuwa serikali ya CCM itatekeleza miradi mingine ya maendeleo ikiwemo skimu nne za umwagiliaji, ujenzi wa masoko ya mazao, vituo vinne vya afya, pamoja na shule sita za msingi na shule mbili za sekondari.


Nchimbi amesema serikali ya CCM itaajiri walimu 7,000 na watumishi wa afya 5,000 ili kupunguza changamoto ya upungufu wa watumishi kwenye sekta hizo muhimu huku akiongeza kuwa vijana na wajasiriamali watawezeshwa kupitia mikopo ya shilingi bilioni 2,00 kwa ajili ya kurasimisha biashara zisizo rasmi na kukuza uchumi wa wananchi.


Aidha, mgombea mwenza huyo ameahidi kuwa endapo chama chake kitaaminiwa kupewa uongozi ndani ya siku 100 za mwazo watahakikisha wanawake wajawazito, wazee, wenye ulemavu na watoto watapatiwa huduma ya bima pia kushughulikia kero ya muda mrefu ya Barabara ya Tabora.


Dkt. Nchimbi amewasili Kahama akitokea Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kufungua kampeni za CCM na kusisitiza kuwa chama hicho kitaendelea kuboresha maisha ya wananchi kupitia utekelezaji wa sera na ilani yake.

1000777713.jpg
1000777727.jpg
1000777735.jpg
1000777737.jpg
1000778115.jpg
1000777703.jpg
1000777723.jpg
1000777717.jpg
1000777743.jpg
1000777733.jpg
1000777731.jpg
1000777711.jpg
1000777719.jpg
1000777741.jpg
1000777721.jpg
1000777745.jpg
1000777685.jpg
1000777689.jpg
(Bila tafsiri)

Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe