Katika ukurasa wa Hariri Tovuti (
) ipo sehemu ya Hariri Kurasa, ambayo inaorodhesha kurasa zote za tovuti ya shirika lako. Hapa unaweza kuhariri ukurasa uliyochapishwa, kubadili utaratibu ya ukurasa, au kuongeza ukurasa mpya kwenye tovuti yako.

Kurasa ambzao zinaonekana kwenye tovuti yako zimeorodheshwa kwa rangi nyeusi yaani "bold", juu ya mstari ya kijivu, zitaonekana kwenye utaratibu kama ilivyo katika menyu ya tovuti yako. Ili kuhariri ukurasa, bonyeza jina lake.
Upande wa kulia, kuna "mishale ya zinazolenga juu" ambazo zinakuruhusu kubadili utaratibu wa kurasa katika menyu ya tovuti yako. Kwa kubonyeza mshale, unaweza kusogeza ukurasa kuelekea mwanzo wa menyu ya tovuti yako. Ukurasa uliopo juu ya orodha unatumika kama ukurasa wa mwanzo wa tovuti yako.
Kutegemea na ukurasa unayotaka kuhariri, hatua tofauti zitachukuliwa. Lakini sana sana kurasa nyingi, kama vile Historia, Miradi, na Timu, zina boksi kubwa nyeupe, inayoonekana kama hii:

Katika boksi hii, unaweza kuandika habari na kuingiza picha au hati. Unaweza pia kunakiri na kuhamisha habari kutoka eneo nyingine, kama vile hati za Microsoft Word.
: Kinaumba kiungo na tovuti nyingine, ama kwenye tovuti yako au mahali pengine.
: Kuingiza picha
: Kuingiza faili nzima ya hati, kama vile Microsoft Word, PowerPoint, PDF, n.k.
: Kuhifadhi mabadiliko yako (bila kuyachapisha), ili usipoteze kazi yako.
: Kurudisha ukurasa wako kwa toleo la awali.
Kuongeza Kurasa Mpya
Katika ukurasa wa Hariri Tovuti (
), chini ya sehemu ya Hariri Kurasa kuna orodha ya kurasa zilizopendekezwa uziongeze kwenye tovuti ya asasi yako, na pia kipengele cha Ongeza ukurasa mwingine, ambacho kinakuruhusu kuongeza ukurasa wowote unaotaka.
Wakati unapobonyeza Ongeza ukurasa mwingine, hatua inayofuata ni kuchagua jina la ukurasa litaloonyeshwa katika menyu ya tovuti yako, na kisha kuongeza maandiko (na picha) kwenye ukurasa wako mpya. Mwishoni, bonyeza kitufe cha Umba ukurasa ili kuchapisha ukurasa wako mpya katika tovuti yako.

Njia nyingine kwa Kuhariri Kurasa
Ukiwa umefungua tovuti yako ya Envaya, unaweza kubonyeza Hariri Ukurasa iliyopo upande wa kulia juu ili kuhariri ukurasa, kama hapo chini:

Kufuta Kurasa
Ukitaka kuondoa ukurasa kutoka tovuti yako, kwanza, fuata hatua hapo juu ili kuhariri ukurasa. Kisha, bonyeza kitufe chekundu cha Futa ukurasa, kama hapo chini: 