Base (Swahili) | Kiswahili | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Lindi non governmental organisation network ilianzishwa kama Mtandao wa asasi za kiraia wa wilaya mwaka 2002 kufuatia warsha ya asasi za kiraia 13 za wilaya ili kubaini na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazokabili sekta ya AZAKi katika kufikia malengo yao.kwa msaada mkubwa wa shirika la kigeni lijulikanalo kama THE CONCERN WORLDWIDE Lindi non governmental organisation network(LINGONET) ilianzishwa na kusajiliwa rasmi mwaka 2003 na kupata cheti cha ithibati(certicate of compliance) mwaka 2010 Saidi Kawanga, Mhasibu
Khamis Chilinga, Katibu Mtendaji Bi Esha Salum ,Mwenyekiti wa LINGONET .LINGONET inaendeshwa kwa taratibu za uanachama,asasi yoyote iliyosajiliwa katika sheria za NGOs inaweza kuomba na kuingia uanachama wa LINGONET malengo makubwa ya LINGONET ni kujenga uwezo wa asasi katika wilaya ya LINDI,kuratibu shughuli zao ili kuepuka muingiliano wa shughuli na kujenga uwezo wa jamii katika kuandaa,kupanga na kutekeleza miradi ya maendeleo na uchambuzi wa sera LINGONET imefanya shughuli kadhaa katika kujenga sekta ya AZAKi katika wilaya ya Lindi tangu kuanzishwa kwake kwa ufadhili wa mashirika mbalimbali kama ifuatavyo; (i) Mradi wa CODEP ambao ulilenga kujenga uwezo wa asasi za kiraia katika kushirikiana na kuboresha mahusiano na wadau wengine wakiwepo serikali kwa ufadhili wa THE CONCERN (ii) Mradi wa kujenga mitandao ya wilaya katika mkoa wa Lindi mwaka 2006-2007 kwa ufadhili wa The Foundation for civil society (iii) mradi wa kujenga uwezo wa AZAKi na wananchi katika ushawishi na utetezi juu ya uchambuzi wa sera.mwaka 2009-2012 kwa ufadhili wa The Foundation for civil society (iv) mradi wa haki na usawa wa kiuchumi unaofadhiliwa na SIDA kupitia kwa SAVE THE CHILDREN kwa miaka maradi ambao unalenga kujenga uwezo wa watoto katika kutambua na kudai haki zao kupitia mabaraza ya watoto yaliyoundwa katika kata na wilaya zote za wilaya za Kilwa ,Lindi na Ruangwa mradi huu ni wa miaka minne LINGONET inapata viongozi wake kupitia uchaguzi inaofanyika mara moja kila baada ya miaka mitatu ambapo viongozi wafuatao huchaguliwa (1) Mwenyekiti (2) Makamu mwenyekiti (3) Katibu mtendaji (4) Katibu msaidizi (5) Mweka hazina (6) Wajumbe saba(7) LINGONET imeweza kuratibu uanzishwaji wa mtandao wa mkoa wa lindi LINDI ASSOCIATION OF NGOs(LANGO) kupitia mradi wake wa kujenga uwezo wa mitandao na kwa sasa inafanya kazi ya kujenga uwezo wa asasi ili ziweze kujiendesha kwa ufanisi na kufikia malengo yao katika kuhudumia jamii LINGONET inaratibu mradi wa haki na usawa kiuchumi katika wilaya tatu za mkoa wa Lindi,mradi ambao unatekelezwa katika wilaya saba za Tanzania za Temeke,Kilwa,Ruangwa,Lindi,Same,Handeni na Arusha kwa ufadhili wa SIDA kupitia SAVE THE CHILDREN Hadi hivi sasa LINGONET ina wanachama 23 na maombi kadhaa yanapitiwa kamati tendaji,LINGONET ni mtandao ambao umejijengea jina katika jamii. Picha kubwa juu ni jengo ilipozaliwa LINGONET mwaka 2002,picha kubwa chini ni Mwenyekiti wa kwanza wa LINGONET Mr Said Kawanga,chini yake ni washiriki wa moja ya mafunzo ya LINGONET chini yake ni Mwenyekiti wa sasa wa LINGONET Bi Esha Salum na mwisho chini ni Katibu Mtendaji wa sasa wa LINGONET Mr Khamis Chilinga
|
(Not translated) |