Base (Swahili) |
Kiswahili |
NURU HARISI WAENDELEA KUTOA ELIMU KWA MAMA NA BABA LISHE
DIRA YETU NI KUWAWEZESHA WAUZA VYAKULA NA MATUNDA WAZINGATIE YAFUATAYO ILI KUEPUKA KUENEA KWA KIPINDUPINDU KWA WATEJA
- Osha vyombo kwa maji safi na sabuni
- Kufunika vyombo vyote vizuri na kwa usafi
- chemsha au tibu maji yote ya kunywa na kutengenezea juisi ya wateja na yafunikwe wakati wote
- Mpe mteja wako chakula kikiwa cha moto
- Weka chombo chenye maji na sabuni kwa kunawia mikono kwa wateja wako
- Nawa mikono kwa maji yanayo tiririka na sabuni baada ya kutoka chooni na kabla ya kuandaa chakula
- Tayalisha chakula katika mazingira safi
- Osha matunda na mbogamboga zisizo chemshwa kwa maji salama
Epuka na pia usichangie kuenea kwa kipindupindu mteja wako akifa kesho utamuuzia nani?
TUNZA AFYA YA MTEJA WAKO.
|
|