Fungua

/dhahabu/history: Kiswahili: WI000D224CDE1E5000006710:content

« Iliyotangulia   ·   Ifuatayo »
Asili (Kiswahili) Kiswahili

 

 

 

 

Dhahabu Arts Group ni Shirika lisilo la kiserikali lililoanzishwa mwaka 2002 na baadae kusajiliwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto. Tokea hapo imekuwa ikifanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa na dira, dhima, lengo na madhumuni yafuatayo:-

1. DIRA

Kuiona jamii ya kitanzania ikiwa bora na uelewa katika afya, elimu, uchumi, utamaduni, mazingira, jinsia na utawala bora.

 

2.  MISSION

Kuiwezesha jamii ya kitanzania katika njia shirikishi kutambua matatizo waliyonayo na kupanga mikakati ya kukabiliana nayo na kuitekeleza kulingana na rasilimali zilizopo.

 

3. LENGO

Kuijenga jamii bora ya kitanzania iliyo bora  zaidi kiafya, kielimu, kiuchumi, kiutamaduni, katika Utawala bora, kijinsia, kimazingira kulingana na viwango vya malengo ya Milenia na sera za kitaifa.

 

4. MADHUMUNI 

(a)     Kutoa elimu ya uwezeshaji kwa jamii na kukuza uelewa katika masuala mbalimbali yaliyo katika lengo na dira yetu (afya, elimu, uchumi, utamaduni, mazingira, jinsia na utawala bora)

(b)     Kushirikiana na mashirika mbalimbali yenye lengo kama letu katika ujenzi wa nguvu za pamoja ili kuiwezesha jamii kuwa bora katika sekta zote.

(c)     Kuandaa, kuingia/kujiunga na kushiriki katika Kampeni mbalimbali za kupigania maendeleo ya wananchi  wa kawaida na  na makundi yaliyoacha/kuwekwa pembezoni.

(d)    Kuhakikisha Jamii, viongozi, Asasi na makundi ya kijamii vinakuwa na ufahamu kuhusu utawala bora na nafasi yao kikatiba ili kuweza kushiriki katika matukio mbalimbali ya kidemokrasia ili kutimiza haki yao ya kikatiba waliyonayo.

(e)     Kuhakikisha Tanzania na Dunia panakuwa mahala bora zaidi pa kuishi.

 

(Bila tafsiri)

Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe