Envaya

/chavitakondoa: Kinyarwanda: WI000493DCC2254000089519:content

Base (Igiswayire) Kinyarwanda
  • UTUME WA CHAVITA-MISSION

  

CHAVITA itahakikisha kuwa jamii ya viziwi ina maisha bora, inayojijengea uwezo wa kujiamini, kujithamini, kujiendeleza, kukuza lugha ya alama ya Tanzania na kushiriki kikamilifu katika shughuli zote za kimaendeleo, kiuchumi na kijamii kwa kushirikiana na serikali na taasisi nyingine.”

                                                      

  • DIRA YA CHAVITA-VISION

  

CHAVITA itahakikisha kuwa jamii ya watanzania inawatambua, inawakubali, inawathamini, inawashirikisha viziwi na kuhakikisha hawasumbuliwi na umasikini, unyanyasaji, ubaguzi na ukandamizaji wa aina yoyote”

 

  1. MALENGO YA CHAVITA

 

Kama wanajamii, viziwi wanayo haki ya kuchangamana na watu wengine na kushirikishwa kikamilifu katika shughuli za jamii. Hii ni haki ya msingi ya binadamu. CHAVITA itahakikisha hili kwa:

 

  • Kuhamasisha matawi ya CHAVITA na jamii ya Viziwi popote walipo hapa Tanzania, jamii ya watanzania, taasisi na serikali kuhusu haki za Viziwi.
  • Kupigania usawa katika fursa za elimu, huduma za jamii na nyanja zote za maisha ya binadamu.
  • Kupigania kutambulika kisheria kwa Lugha ya Alama ya Tanzania.
  • Kujenga mwamko na kukuza matumizi ya Lugha ya Alama kwa matawi ya CHAVITA, jamii ya Viziwi nchini, na kwa jamii ya watanzania kwa ujumla.
  • Kuhakikisha shughuli za maendeleo ya jamii na ki-uchumi kwa matawi ya CHAVITA na jamii ya Viziwi nchini zinaboreshwa.
  • Kuhakikisha matawi ya CHAVITA na jamii ya Viziwi nchini wanapata uwakilishi katika ngazi zote za uongozi.
  • Kufanya na kuendeleza utafiti kuhusu masuala yanayowahusu Viziwi
  • Kupambana na Virusi vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI pamoja na majanga mengine yanayowakabili Viziwi.
(Not translated)

Kugirango ugire icyo uhindura kubyo wasemuye, ugomba kwinjira mu rubuga Injira · Iyandikishe