Injira

/chawaumavita/history: Kinyarwanda: WIcWWXKEU8NE9Yqam47eibOe:content

« Inyuma   ·   Ahakurikira »
Base ((ururimi rutazwi)) Kinyarwanda

Sisi  Wazazi wa Watoto wenye Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo na Viungo tunaopata huduma katika Hospitali na vituo vya  CCBRT tumeamua, baada  kupata semina kuhusu ulemavu wa mtindio wa ubongo akili na wa viungo tarehe 21/04/2012 katika Hospitali ya CCBRT Msasani ambapo pamoja na mambo mengine washiriki walijifunza kuhusu chanzo cha Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo na viungo, tiba na malezi kwa ujumla; 

kuunda chama kitakachosimamia haki za watoto wenye ulemavu wa mtindio wa Ubongo na Viungo, kisajiliwe na baadae kuingia katika kampeni kubwa ya kuona haki za watoto/watu wenye ulemavu wa mtindio wa ubongo na viungo zinapatikana na jamii inakuwa na uelewa na inashiriki katika kuzipigania na kuziboresha na kuhakikisha zinapatikana.

hii ni kwa kuwa vitendo vya ukiukwaji wa haki za Binaadamu kwa watoto wenye ulemavu wa Mtindio wa ubongo, akili na viungo vimekuwa vikishamiri nchini, 

Na kwa kuwa baadhi ya wazazi wamekuwa wakifarakana,  kukimbiana, na hata kumtelekeza mtoto na pia wakati mwingine kumdhuru mtoto mwenye ulemavu baada ya mtoto huyo kuzaliwa au kupatwa na ulemavu baadaye,

Na kwa kuwa kumekuwa na dhana potofu iliyotawala katika jamii juu ya upatikanaji wa watoto wenye ulemavu wa mtindio wa ubongo,akili na viungo na maisha yao kwa ujumla ,

Na kwa kuwa hakuna huduma za awali kabla na baada ya tatizo zilizo endelevu zitolewazo kwa watoto wenye mtindio wa ubongo,akili na Viungo kwa watoto/watu wanoishi na ulemavu huo,

Na kwa kuwa mipango na mikakati  iliyopo nchini haikidhi changamoto zinazoendelea kujitokeza   kwa watoto/watu wenye ulemavu wa mtindio wa ubongo,akili na  viungo nchini,

Na kwa kuwa  mtoto mwenye ulemavu ni sawa na mtoto mwingine yeyoteanastahili kupata huduma na vifaa tiba maalum vya matibabu, na nafasi sawa ya elimu na mazoezi ili kumsaidia kufikia malengo yake ya kimaisha,

Na kwa kuwa sisi wazazi na wananchi kwa ujumla tuna jukumu la awali la kuhakikisha  kuwa watoto/watu  wenye ulemavu wa mtindio wa Ubongo na Viungo wanakuwa salama na duniani panakuwa ni mahala bora pa kuishi kwao;

 

MAFANIKIO 

Mara baada ya kubainisha malengo ya uanzishwaji wa chama,hatimaye harakati zilianza katika kufuatilia usajili,wakati mchakato wa usajili ukiendelea tuliweza kujitambulisha wizara ya afya na maendeleo ya jamii,kitengo cha maendeleo ya jamii,kilichopo jirani na  stendi ya akiba jengo la PPF.

HATIMAYE baada ya kujitambulisha tuliweza kualikwa katika ugawaji wa iti vya walemavu hasa watoto wenye umri chini ya miaka 12 na juu ya miaka 4.msaada huu ulitolewa na mama Anna Mkapa kijiji cha makumbusho kupitia kwa wafadhili /wahisani kampuni ya madini

 UTAONA NDANI ya muda mfupi chama kimejitahidi kusimamia malengo.pia mwezi uliopita tumeweza kupata rasmi usajili kupitia msajili wa vyama vya kiraia CSO-wizara ya mambo ya ndani na usalama wa raia-msajili wa vyama-

 

 

 

 

(Not translated)

Kugirango ugire icyo uhindura kubyo wasemuye, ugomba kwinjira mu rubuga Injira · Iyandikishe