Envaya

/woy/news: English: WI0007C234C83F8000001649:content

Base (Swahili) English
Ripot ya mafunzo ya kazi za mikono Vijana Simama Imara WOY Moshi
Utangulizi
White Orange inatekeleza mradi wa vijana simama imara. Mradi huu umefadhiliwa na SATF na una lengo la kuboresha maisha ya vijana wanoishi katika hali duni kwa kuwapa stadi za kazi na stadi za maisha.
Kwa zaidi ya miezi sita WOY imekuwa ikiwafundisha vijana elimu ya kazi ya mikono ambapo wastani wa watoto 25 wamekuwa wakikutana kila jumamosi kwa ajili ya mafunzo haya. Hadi kufikia sasa VSI wamejifunza jinsi ya kutengeneza mikufu, vikuku, hereni na urembo mbalimbali kwa kutumia shanga za masai, miti na mbegu za mimea. Vile vile wamejifunza kutengeneza nyumba za asili kwa kutumia majani na udongo.
Jinsi mafunzo yanavyoendeshwa
Wanafunzi hujifunza kwa kuona, kuelekezwa na kutengeneza ambapo mkufunzi huleta bidhaa ambayo iliyokwisha tengenezwa au picha ya bidhaa na kisha kuaelekeza VSI jinsi ya kutengeneza (kushika uzi, sindano na jinsi ya kupangilia rangi) kisha VSI hujaribu kutengeneza na kurudia mara kwa mara hadi watakapokuwa wameelewa.
Mafanikio
VSI kwa kushirikia na wakufunzi wao wametengeneza bidhaa nyingi ambapo huuza katika matukio mbalimbali
Malengo ya baadaye
VSI wakisha kuwa na umahiri katika ufundi huu, watafundiswa sanaa nyingine ikiwemo kusuka midoli, mifuko rafiki ya mazingira na kutengeneza kadi za migomba.
Wakufunzi
Upendo Mkufunzi mkuu
Jema Mkufunzi Msaidizi
Mrs Nyata- Bibi

Taarifa ya mafunzo ya uongozi yaliyotolewa kwa VSI katika ukumbi wa ofisi ya WOY Moshi
Utangulizi
Kwa msaada kutoka SATF White Orange Youth wanatekeleza mradi unaitwa ‘Vijana Simam Imara’ Mradi huu umeanzishwa kwa kujifunza mafanikio ya mfano kwa shirika la Humuliza linalopatikana kanda ya ziwa Victoria. Shughuli ambazo WOY wanafanya katika mradi huu ni pamoja na kuwafundisha vijana elimu ya uongozi na stadi za maisha Katika mwezi wa Mei WOY ilifanya mafunzo ya Stadi za maisha na Uongozi kwa VSI. Mafunzo haya yalifanyika kwa muda wa siku tatu ambapo jumla ya watoto 26 waliudhuria. Mafunzo haya yalifanyika katika ofisi za WOY zilizopo majengo.
Lengo la mafunzo
Mafunzo haya yalilenga kuwajengea uelewa VSI kueliwa maana ya uongozi, aina mbalimbali za uongozi na sifa za kiongozi bora.
Mwezeshaji alielezea kwamba uongozi ni dhana ambayo humpa mtu dhamana ya kutawala au kuongoza watu au makundi Fulani pia alielezea kwamba uongozi/viongozi wapo wa aina mbalimbali kama wafuavyo
• Viongozi wa kuchaguliwa- Ilielezewa kwamba viongozi wakuchaguliwa huchaguliwa na watu. aidha kwa kutumia kura au chaguzi za watu kutokana na sababu zao
• Viongozi wa kuteuliwa- Ilielezewa kwamba aoina hii ya uongozi, viongozi husika huteuiwa kutokana na mamlaka mbalimbali kwa mfano wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa ambao huteuliwa na mamlaka za juu za serikali aidha kutokana na uzoefu wao wa muda mrefu au kutokana na sababu nyinginzo muhimu. Mwezeshaji alielezea kwamba zipo aina mbalimbali za uongozi kama ifutavyoongozi wa
Uongozi wa kidemokrasia
Ilielezwa kwamba uongozi wa kidemokrasia ni ule unaopatikana kwa njia ya kidemokrasia na kwamba njia pekee ya kupata uongozi/viongozi ni kwa kufanya uchaguzi uio huru na haki. Pia uongozi wa kidemokrasia unaweza kupatikana kwa kuteuliwa na viongozi waliochaguliwa kidemokrasia kama zinavyoeleza katiba na sheria za nchi.
Uongozi wa kidikteta
Mwezeshaji alielezea kwamba uongozi wa kidikteta ni ule unaopatikana kwa kutumia mabavu. Njia hizi ni pamoja na zile za kufanya mapinduzi ya kijeshi. Kadhalika kiongozi anaweza kupatikana kwa njia ya uchaguzi wa kidemorasia lakini baadaye akawa hatawali kwa kufuata misingi ya kidemokrasia ikiwa ni pamoja na kutofuata sheria, kanuni, taratibu na sheria zilizopo. Mwezeshaji aliwaeezea washiriki kwamba kiongozi anatakiwa awe na sifambalimbali ambazo ndizo zinazomwezesha kukubalika na watu au makundi aya watu anayowaongoza katika ngazi mabalimbali. Sifa hizo zilielezewa kama ifuatavyo:
1. Anapaswa awe muwazi
2 .Anapaswa awe mwenyekuheshimu mawazo ya watu wengine
3 .Anapaswa awe mwaminifu
4 .Anayekubalika katika jamii
5 .Awe na uwezo wa kupngoza
6 .Awe mkweli na
7 .Akubali kukusolewa na
8 .Asiwe na jazba
Baada ya kuwasilisha somo hili la uwongozi, mwezeshaji aliwaelezea washiriki kwamba, ili kuwa kiongozi bora ni lazima kuzingatia sifa tajwa hapo juu ili aweze kukubaika na watu au mamlaka mbalimbali. Baada ya somo hili kumalizika washiriki waliuliza maswali mbalimbali ambayo yalijibiwa. Washiriki waliitimisha kwa kusema kwamba somo limeeleweka na kufuata sifa hizo ili wawe viongozi bora wa siku zijazo.
Igizo
Watoto waligawanywa katika makundi mawili, kundi A lilifanya igizo la uongozi usio bora, na kundi B likafanya igizo la uongozi bora. Baada ya maigizo haya mwezeshaji alianzisha mjadala kwa kuuliza maswali watoto kwamba ni uongozi gani wangeupenda na ni sababu zipi zilizowafanya wapende aina hiyo ya uongozi.
Wawezeshaji
Raphael Waitta
Gamaliel Mbaase
Orodha ya washiriki
1. Mwanahawa M Shayo
2. Mwajuma Bakari
3. Mariamu juma
4. Halima Hashimu
5. Zainabuu Hashimu
6. Magreth Robinson
7. Aviti Mustafa
8. Anjiti Mustafa
9. Niteshi Mustafa
10. Rashidi Issa.
11. Deo Frank
12. Japhet Yohana
13. Stivin Dobald
14. Merry stephano
15. Josephine JAMES
16. John Godfrey
17. Athumani Gabon
18. Mapinduzi Ally
19. Bakari hasani
20. Hamza Mudy
21. Lydia Joseph
22. Elizabeth Gasper
23. Amani Raphael
24. Swahumu Isa
25. Merry Stephano
26. Lillian Alex
Ripot job training of Youth Stand Strong hands WOY Moshi
Introduction
White Orange Youth is implementing a project to stand firm. This project was funded by the SATF and aims to improve the lives of young people living in slum conditions by giving them work skills and life skills.
For more than six months has been ikiwafundisha WOY youth education work of the hands where approximately 25 children have been met every Saturday for this training. VSI Until now have learned how to make chains, bracelets, and beauty range hereni using Masai beads, wood and seeds of plants. Similarly, they have learned to make traditional houses using straw and clay.
How training yanavyoendeshwa
Students learn to see, directed by forming when the trainer brings a product which iliyokwisha made or a picture of the product and then kuaelekeza VSI how to make (to keep the yarn, needles and how to configure color) and VSI tries to create and repeat frequently until you are understood.
Achievements
VSI to kushirikia and their trainers have developed many products which are sold in various events
Future goals
VSI, when they have technical competence in this art will fundiswa other toys, including braiding, environmental friendly bags to make banana cards.
Trainers
Loving great trainer
Good Tutor Assistant
Mrs. Bibi will be-

Information provided leadership training for VSI in the hall of the office in Moshi WOY
Introduction
With help from SATF White Orange Youth are implementing a project called 'Youth Simam Stable' This project has been initiated to study the success of the model for the organization of Humuliza found the lake Victoria region. WOY activities that are performed in this project include education and teach youth leadership and life skills in the month of May WOY conducted life skills training and leadership for the VSI. This training was held for three days where a total of 26 children had attended. This training took place at the offices of WOY existing buildings.
The goal of training
This training focused on building awareness for VSI kueliwa leadership, various kinds of leadership and qualities of leadership.
The facilitator explained that leadership is a concept which gives a bond to dominate or lead the people or certain groups also explained that the leadership / leaders are as diverse wafuavyo
• elected officials-wakuchaguliwa was explained that the leaders are elected by the people. either by using the voting or elections due to their
• Leaders of appointment-was explained that aoina this leadership, the leaders concerned are teuiwa from various authorities for example, heads of districts, heads of provinces, who are appointed by authorities on the government either because of their experience of long term or due to nyinginzo important . The facilitator explained that there are different kinds of leadership as ifutavyoongozi
Democratic leadership
It was mentioned that the democratic leadership is acquired by democratic means and that the only way to get leadership / leaders is to make the elections free and fair purpose. Also, democratic governance can be found for appointments and democratically elected leaders like zinavyoeleza constitution and laws of the country.
Dictatorial leadership
The facilitator explained that the dictatorial leadership is acquired by the rule. These include those for making a coup. Likewise, the leader can be found through kidemorasia election but they later became not to follow democratic principles, including instructions, rules, regulations, procedures and existing laws. The facilitator was waeezea participants that the leader should be and I fambalimbali zinazomwezesha which are accepted by individuals or groups to a paragraph is yowaongoza people at various levels. These characteristics zilielezewa as follows:
1. He should be open
2. He should have thought of other people mwenyekuheshimu
3. He must be faithful
4. Anayekubalika community
5. Should be able to kupngoza
6. Should be honest and
7. Agrees to kukusolewa
8. Let it be the feeling
After presenting this lesson guide, a facilitator was explained to participants that, in order to become a better leader must consider the above characteristics in order to kukubaika to persons or authorities. After completion of this study participants were asked various questions which yalijibiwa. Participants itimisha to say that subject to compliance limeeleweka these qualities to become better leaders of the future.
Scenario
Children were divided into two groups, group A carried out an outstanding leadership role, and group B likafanya role of leadership. After this drama facilitator initiated the discussion by asking questions that are leading the children what they wanted and what reason is' hooked on that kind zilizowafanya...

In order to edit translations, you need to log in. Log in · Register

Translation History

Google Translate
March 21, 2011
Ripot job training of Youth Stand Strong hands WOY Moshi – Introduction – White Orange Youth is implementing a project to stand firm. This project was funded by the SATF and aims to improve the lives of young people living in slum conditions by giving them work skills and life skills. – For more than six months has been ikiwafundisha WOY youth education work of the hands where approximately 25 children have been met every Saturday for this training. VSI Until now have learned how...