Envaya

/teyoden/post/717: Kiswahili: WI0008A5B034EE0000000717:content

Asili (Kiswahili) Kiswahili
Vijana wa TEYODEN wajadili ukimwi kwa kina

Katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili vijana hapa nchini,vijana wa TEYODEN hivi karibuni walipata fursa ya kuyaunganisha mawazo yao kwa njia ya mjadala kuhusiana na ugonjwa wa ukimwi ikiwa ni katika mfululizo wa mijadala inayofanyika mara mbili katika kila mwezi.
Katika mjadala huo vijana waliona ni muhimu kukawepo na wataalamu toka idara ya afya,viongozi wa dini na ikiwezekana awepo kiongozi mmoja toka serikalini,kwani mara nyingi umekuwepo mgongano wa matumizi ya kondomu kwa wale wanaohitaji kufanya hivyo wakati huo huo viongozi wa dini wanalipinga hilo.
Na katika kupingana huko kumesababisha wanaharakati kuonekana kama wanatoa mafundisho yaliyo kinyume na maadili ya dini.
Pia kuna changamoto nyingine iliyoibuliwa na vijana hao hususani pale wanapopata mafunzo kutoka TEYODEN huwa hawapewi vyeti vyenye kuonyesha ushiriki wao,na katika hilo uongozi wa TEYODEN umelikubali hilo na utalifanyia kazi mara moja.Sambamba na hilo pia kulipendekezwa kuwepo kwa vitambulisho kwa vijana wote wa TEYODEN katika kata zao ikiwa ni sehemu ya kujitambulisha kwao kwa jamii.
Kila jumamosi ya pili na ya mwisho wa mwezi vijana hawa hukutana na kufanya mijadala kuhusu mambo mbalimbali yanayowahusu.
(Bila tafsiri)

Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe