Fungua

/sawaka/projects: Kiswahili: WI0004F30CFE6BE000002253:content

« Iliyotangulia   ·   Ifuatayo »
Asili (Kiswahili) Kiswahili

 

SAWAKA ni shirika linalojitegemea lisilo la kiserikali (NGO) lilioanzishwa mwaka 1995 na kuandikishwa chini ya sheria ya uandikishaji mashirika ,NGO Act , No 24 ya mwaka 2002 .Tangu kuanzishwa kwake shirika hili limekuwa likijishughulisha na utaoaji wa huduma mbali mbali kwa jamii na hasa wazee na makundi mengine ya watu wasiojiweza Kama vile watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu ,wajane na watu waishio na Virus vya UKIMWI.Baadhi ya shughuli ambazo zimekuwa zinatekelezwa na shirika hili katika mwaka 2009 ni pamoja na :-

  • Ujenzi na ukarabati wa nyumba za wazee wasiokuwa na uwezo na wale wanaotunza watoto yatima na wagonjwa waishio na VVU
  • Mafunzo kuhusu haki za watoto ,wazee na stahiki zao kama zinavyoanishwa katika Sera mbali mbali na miongozo ya kitaifa na mipango ya maendeleo kama MKUKUTA n.k
  • Huduma ya Misaada ya dharula ( Chakula ,mavazi ,vyombo vya ndani ,matandiko,vyandarua  n.k) kwa wazee maskini wasiokuwa na uwezo kupitia mradi wa SAG.
  • Uanzishaji wa Miradi midogo midogo ya uzalishaji kwa ajili ya kuinua kipato cha kaya maskini za wazee na wategemezi wao.
  • Mradi wa Jali watoto ( huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu) kama vile Elimu, Msaada wa kisaikolojia ,Afya , Chakula na lishe ,malezi bora ya watoto, Malazi na makazi ,n.k)

1.0    MAFANIKIO

1.1   Uanachama  

Katika mwaka huu wamajiunga wanachama wapya wa SAWAKA 434 toka katika vijiji mbali mbali . Mwanzoni mwa mwaka tulikuwa na wanachama hai 1,467  na hivyo kufikia mwishoni mwa mwezi Desemba 2009 SAWAKA ilikuwa na wanachama hai 1,901 . Aidha ,tulipata michango ya kiingilio Tshs 434,000/= na ada ya mwaka Tshs 715,500/= na jumla ya matawi hai 25 tu.

 

1.2    Mradi  wa kusaidia wazee wasiokuwa  na uwezo wanaofadhiriwa na Sponsor a Grand Parent program (SAG). 

Mradi huu ambao unatekelezwa katika vijiji vya Kagenyi, Rwabwere na Iteera  unafadhiriwa na Shirika la HelpAge International toka mwaka 1998 ,na katika mwaka 2009  tumetekeleza yafuatayo;-.

 

o        Ujenzi wa nyumba kwa wazee wasiojiweza . 

Jumla ya nyumba 5 zenye thamani ya Tshs 9,425,000 zilizokuwa zinakaliwa na wazee wasiojiweza na wategemezi wao zimeweza kukarabatiwa na kujengwa upya .  Mojawapo ya nyumba zilizojengwa mwaka huu katika mpango huu ni pamoja na nyumba ya mzee Zeulia Philmelick kama inavyoonyesha hapa chini.

 

 

Nyumba ya awali ya Bi  Zeuria Philmelki ilivyokuwa .

 

 

Nyumba mpya aliyojengewa Bi Zeuria Philmelick

 

 

 

 

 

 

 

 

 

o        Utoaji wa huduma muhimu za msingi kwa wazee wanaofadhiriwa na mradi huu .

 

Katika kipindi hiki tuliweza kuwasaidia watoto yatima 61 wanaolelewa na wazee katika kata za Rwabwere na Kiruruma kwa kuwapatia sare za shule ,vifaa vya shule na viatu ili kuendelea na masomo . Wazee 281 ( wanawake 137 na wanaume 144 ) walipatiwa vyandarua na wategemezi wao 671 .

 

o        Miradi ya kiuchumi.

 

Katika kutekeleza mradi huu tumekuwa tukihamasisha wazee kuanzisha vikundi vya wazee kwa ajili ya kuanzisha miradi ya kiuchumi. Jumla ya vikundi 3 vya wazee vimeundwa mwaka huu na vinaendesha shughuli za ufugaji wa nyuki ,ufugaji wa mbuzi na kilimo cha bustani ya nanansi.

 

 

 

 

 

2.2)         Huduma kwa watoto walio katika mazingira hatarishi chini ya mradi wa Jali watoto.

Mradi huu unafadhiriwa na Shirika la USAID la nchini Marekani kupitia PACT (TZ) kupitia SAWAKA na HelpAge Intarnational katika wilaya ya Karagwe . Mradi huu ambao ulikuwa wa miaka 2 na ulitarajiwa kuishia mwezi November 2008 na tulibahatika mradi huu kuongezewa mkataba wa miaka 2 hadi December 2010. Aidha ,kwa mwaka huu tumeweza kuhudumia watoto walio katika mazingira magumu zaidi katika nyanja zifuatazo;-

Aina ya huduma

Idadi ya watoto waliofikiwa

Elimu ( Sare, Karo na vifaa vya shule).

Jumla ya watoto 109  wa sekondari walilipiwa karo na mahitaji mengine ya shule

Afya (kadi za bima ya afya)

Watoto yatima 1,374 na walezi wazee 590 kupitia Halmashauri ya wilaya Karagwe ambapo SAWAKA ilichangia Tshs 10 milioni.

Msaada wa Kisaikolojia katika vikundi 7

1,291

Mafunzo juu ya malezi bora kwa watoto

1,291

Miradi ya kuimarisha kipato cha familia kupitia miradi ya ufugaji wa mbuzi ,kuku na nguruwe

Mbuzi 315 waligawia katika kaya 279 zenye watoto 572 ,

kaya 10 waligawiwa nguruwe 20

Kaya 158 walinufaika na mgawo wa kuku  wawili wawili kila kaya

 

Here are pupils from Nyakagoyagoye primary school looking happy and well dressed after receiving school uniforms and material from the project.

 

 

Picture by staff, SAWAKA 2009

 

 

 

 

 

  

 

 

Watoto waliosaidiwa sare 2009

 

S/No

Village

Male

Female

Total OVC

1

Kafunjo

7

8

15

2

Karongo

4

7

11

3

Chanya

6

4

10

4

Nyakahanga

5

5

10

5

Bisheshe

3

7

10

6

Omurusimbi

2

3

5

 

Total

27

34

61

 

 

Wakati huo watoto 109 wanaosoma shule za kutwa za sekondari walilipiwa karo na ada ya mitiahani.

 

 

Table 2; Watoto waliosaidiwa mwaka  2008.

 

S/No

Village

Male

Female

Total OVC

1

Kiruruma

7

11

18

2

Kamagambo

8

10

18

3

Nyakagoyegoye

4

10

14

 

Total

19

31

50

 

 

 

 

 

 

 

Table 3; Watoto waliosaidiwa  2007

S/No

Village

Male

Female

Total OVC

1

Kiruruma

7

11

18

2

Kamagambo

8

10

18

3

Nyakagoyagoye

4

10

14

 

Total

19

31

50

 

 

1.3    Ushawishi na utetezi kuhusu haki na stahiki za wazee

Shughuli hii imeendelea kufanyika katika kata za mfano za Nyakahanga ,Kiruruma na Rwabwere .Lengo la shughuli hii ni kuwawezesha wazee kuzifahamu stahiki na haki zao kama zinavyoanishwa katika sera mbali mbali za kitaifa ( Sera ya afya ,Sera ya wazee ,sera ya maji ,Sera ya Taifa ya UKIMWI ) na MKUKUTA.

Aidha ,vikundi vya ufuatiliaji wa haki hizi vimeundwa na mafanikio yake ni kwamba katika kata hizo wawakilishi 2 wa wazee wameunganishwa katika kamati za maendeleo za kata ili kuwakilisha mawazo ya wazee .

Pia shughuli hii imesaidia kuongeza uelewa miongoni mwa viongozi muhimu katika ngazi ya wilaya kuhusu masuala ya uzee na kuzeeka na baadhi ya miradi ya wazee imeingizwa katika program za maendeleo ya wilaya kama TASAF. Miradi ambayo kwa mwaka huu imekubaliwa na TASAF ni pamoja na Mradi wa ujenzi wa klabu ya wazee katika kijiji cha Bisheshe umegharimu kiasi cha Tshs 12 million na ule wa Bustani ya miti uliogharimu kiasi cha Tshs 6,850,000.=  wa kikundi cha wazee Kayanga . Mradi huu wa Bustani umeanza kutekelezwa kwa awamu ya kwanza jumla ya miche 39,855 hadi mwishoni mwa mwezi December 2009 ilikuwa imeoteshwa tayari kwa ajili ya kuuzwa.

 

 

1.4  Uanzishaji wa Miradi midogo midogo ya uzalishaji kwa ajili ya kuinua kipato cha kaya maskini za wazee na wategemezi wao.

Katika kipindi hiki SAWAKA iliweza kuhamasisha uanzishaji wa vikundi vya wazee na kuanzisha miradi mbali mbali kama ifuatavyo;-

S/n

 
(Bila tafsiri)

Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe