Log in

/TEYODEN/post/115507: English: WIs77B0czoTiOleQlXP9VljG:content

« Previous   ·   Next »
Base ((unknown language)) English

 

MABINTI KATIKA KATA ZA AZIMIO, CHARAMBE NA MBAGALA WAPATA MRADI MPYA WA KUWAJENGEA UWEZO.

Mradi mpya wa kuwajengea uwezo mabinti wa umri kati 15-19 umezinduliwa katika viwanja vya Zakhiem.Mradi huu ambao unategemea kutekelezwa kwa ubia kati ya Halmashauri ya Manispaa ya Temeke na Restless kwa kushirikiana kwa karibu kati ya UNICEF na TACAIDS utatekelezwa katika kata za Azimio,Charambe na Mbagala walengwa wakiwa ni wasichana wa umri wa kati ya miaka 15-19 kutoka kata husika.

Mradi kama huu ulifanywa na Mtandao wa Maendeleo ya Vijana Manispaa ya Temeke kwa ushirikiano na Tamasha na ufadhili wa Population Council ukihusisha kata za Azimio,Mtoni,Vijibweni na Kibada.

 Akitoa maelezo Mwenyekiti mtendaji wa TACAIDS bi Fatuma Mrisho aliwaasa wanaume kutoa wanyanyasa wasichana kwa kuwa na haki sawa kama wanaume.Alilisisitiza kuwa hali ni mbaya kwa kuwa maambukizi ni makubwa sana upande wa wasichana.”Karibu robo tatu za walioathirika na maamukizi ya V.V.U ni wasichana,mbaya zaidi karibu asilimia 30 ya wanawake waliowahi kufanya ngono wanaona sawa kufanya ngono kwa kulazimishwa”alisema mama Mrisho.

 Katika nasaha zake Miss Tanzania wa mwaka 2004 Bi Faraja Kota aliwapa moyo wasichana na kuwataka kujitambua na kuwa na dira katika maisha kwa kuwa kila kitu kinawezekana kwao.Aliwashauri wasichana kuwa ngangari na kamwe wasikubali kuchakachuliwa.Faraja alimalizia kwa kusema hata yeye amepata nafasi ya ukamishna wa Tume ya kudhibiti Ukimwi kwa sababu aliona anaweza hivyo wasichana wasikate tamaa na kujirahisisha.

 Kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke bwana Mzirai aliwakaribisha kwa roho kunjufu watekelezaji wa mradi huo Restless development na aliwataka kutumia uzoefu na taaluma za watalaam waliopo katika Manispaa ya Temeke na kata za mradi ili mradi huo uweze kufanya vizuri na kutoa matokeo kama inavyotarajiwa.

Mradi wa Mabinti shika hatamu unategemea kuanza muda wowote baada ya uzinduzi na kwamba wasichana katika kata 3 za mradi wakae tayari kuweza kushiriki katika hatua mablimbali za utekelezaji wake.

  

 

(Not translated)

In order to edit translations, you need to log in. Log in · Register