Asili (Kiswahili) | Kiswahili |
---|---|
MAMBO TULIYOJUMUISHA KWA WIKI HII. kwanza kabisa tunaishukuru serikali kwa kumaliza mgomo wa ma daktari uliodumu takribani wiki tatu.Hii imetufundisha kuwa katika kudai haki ni lazima uchukue hatua zinazokubalika ili chombo husika kiweze kutambua suala husika tumeshuhudia watu walioathirika kwa kiasi kikubwa ni wanawake na watoto,kwani asilimia kubwa ya watoto wanaolazwa ni akina mama ndio wanao wajibika kuwauguza na akina baba wakiwa katika shughuli zao nyingine .Hivyo tunaiomba serikali kushughulikia migogoro mapema baina yake na makundi mbali mbali ili kunusuru akina mama na watoto. Migomo ni dalili ya ukosefu wa haki na usawa wa mgawanyo wa rasilimali tulizonazo,kwa hali hiyo asasi za kijamii na wanaharakati mbali mbali wanatakiwa kufanya kazi ya kuelimisha wananchi na jamii kwa ujumla ili kufahamu haki na usawa wa rasilimali tulizonazo pamoja na mgawanyo wake uko vipi. |
(Bila tafsiri) |
Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe