Base (Igiswayire) | Kinyarwanda |
---|---|
1. Ndiyo serikali ya kijiji ina taarifa na wakati mwingine huwa inawasaidia chakula cha njaa kama kipo. 2. Hana ndugu wa karibu wanaoweza kumsaidia kwani hana baba wala mama na mume wake pia amefariki miaka kama minane iliyopita.Inasemekana kwamba huwa akichanganyikiwa wakati mwingine anawafukuza watoto porini au yeye anaondoka na kupotea hata zaidi ya siku moja nakuwaacha watoto peke yao. Wakati mwingine watoto wanaposahau kufunga mlango wanaingiliwa na fisi na kukimbilia darini hadi asubuhi kwani nyumba ya jirani iko mbali kidogo.Wakiwa darini wanashuhudia mbuzi wao 12 wakiliwa na fisi kwani hawana la kufanya. Wamekuwa wakipata msaada wa serikali ya kijiji lakini si kwa kukidhi haja na hata kutoka kanisa la jirani ambako wanapewa kile kidogo kinachopatikana. Kwa sasa huyu binti yake wa kwanza amefaulu kwenda kidato cha kwanza na kwa mujibu wa taarifa niliyoipata kutoka kwa mwakilishi wetu kutoka huko ni kwamba amerudishwa nyumbani kwa ajili ya kukosa ada na mahitaji muhimu ya shule maana yake hasomi tena. Sisi kama wanaharakati tulibahatika kufika huko kikazi baada ya kumwona na kuelezwa hayo tukaona tumsaidie kumsemea ili watu waweze kumfuatilia huko nasi tuko tayari kuwapeleka kwani sisi tuko Arusha vijijini. Kwa maelezo zaidi huko Bashay kuna mtendaji wa Kata hiyo anapatikana kwa namba 0754315427 au mama martina mosses no. 0766237655 karatu. Ahsante kwa kuguswa kwako na Mungu Akubariki |
(Not translated) |
Kugirango ugire icyo uhindura kubyo wasemuye, ugomba kwinjira mu rubuga Injira · Iyandikishe