Envaya

/jeanmedia/news: English: WI0005164C189A8000007953:content

Base (Swahili) English

JEAN MEDIA, KUPITIA MTWARA FM,REDIO YA JAMII, IMEFUATILIA ATHARI YA MAZINGIRA KUTOKANA NA MABOMU YALIYOLIPUKA KATIKA KAMBI  YA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA KIKOSI NAMBA 511 KATIKA ENEO LA GONGO LA MBOTO JIJINI DAR-ES-SALAAM 

Milipuko mikubwa ya mabomu iliyotokea inchini Tanzania katika ghala kuu la kutunzia silaha la jeshi la wananchi wa Tanzania [JWTZ] Gongo la mboto jijini Dar es salaam imesababisha uharibifu mkubwa wa mazingira.

Milipuko hiyo iliyotokea tarehe 16/02/2011 majira ya saa mbili usiku imesababisha taharuki kubwa na hofu  miongoni mwa wakazi wa jiji la dar es salaam na pia kusababisha watu na wanyama kukimbia huku na huko kujinusuru maisha yao.

Hali kadhalika milipuko hiyo mikubwa imesababisha uharibifu wa mazingira, ikiwa ni pamoja na kupoteza uoto wake wa asili yake, kufuatia moto uliounguza majani. Mabomu yalikata miti na baadhi ya maeneo kutifuliwa, na pia nyumba kuteketea kwa moto.

Uchafuzi wa  mazingira uliosanabishwa na milipuko hiyo, umeathiri mno hali ya hewa na kuichafua kwa kuifanya  kuwa nzito,  kutokana na kuchanganyika na moshi mkali. Vilevile wananchi wanahisi kuwa hewa wanayovuta imechanganyika na sumu,  kwa kile walichokisema kuwa asilimia kubwa ya wahanga miongoni mwao, wanakohoa kwa kipindi kirefu, tangu kutokeee kwa tukio hilo.

Watu ishirini na mbili [22] wamepoteza maisha yao   na wapatao mai tatu[300]kujeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao ,na wengine kupata vilema vya kudumu, kama vile kukosa mikono au miguu, na pia kupoteza sehemu nyingine za miili yao.

Viumbe vingine ni pamoja na wanyama, wadudu na ndege waliopoteza uhai wao katika milipuko hiyo.

kwa mawazo yangu, nadhani kuwa kwa athari zilizo jitokeza katika milipuko hiyo, hapana budi kwa nchi ya Tanzania kutafuta ufumbizi wa haraka, ili kunusuru uharibifu mkubwa wa mazingira utakaoendelea kujitokeza kama mmomonyoko wa udongo, ukosefu wa hewa safi na uchafuzi wa mazingira, ili kulinda afya za jamii na kuboresha maeneo ambayo kabla ya milipuko, yaliyokuwa yakitumika kwa kilimo cha mboga mboga.

NA LEONIA LUCAS MAHONA

 

Jean MEDIA, THROUGH MTWARA FM radio SOCIAL, ENVIRONMENTAL IMPACT FROM IMEFUATILIA and explosives at Camp YALIYOLIPUKA the Tanzanian People's Army forces that 511 IN LA AREA MBOTO staff in Dar-ES-SALAAM

Large explosions inchini Tanzania bombings happened in the main warehouse kutunzia army's weapons are a country of Tanzania [TPDF] mboto staff of Dar es salaam has caused massive environmental damage.

Explosions that happened on 2/16/2011 at two summer night has caused great upset and panic among the residents of Dar es salaam and animals also cause people to run with the power to aid in their lives.

Likewise large explosions that led to environmental degradation, including loss of its natural vegetation, the following fire ounguza leaves. Bombs yalikata trees and some areas kutifuliwa, and also houses ravaged by fire.

The osanabishwa pollution and explosions that you too affects the climate and pollute to make it heavier, and mingle with the smoke from blazing. Similarly citizens felt that the air they breathe and confused among the poison, for what they have said that a large percentage of victims among them, they cough for a long time, since kutokeee for the event.

Twenty-two [22] have lost their lives and about three mai [300] injured parts of their bodies, and others get permanent disabilities, such as missing hands or legs, and also lose other parts of their bodies.

Other creatures include animals, insects and birds who lost their life in the explosions.

to my mind, I think that the effects are appearing in the explosions, therefore, no need for the country to find ufumbizi quickly, in order to save massive destruction of the environment would last appearance as soil erosion, lack of clean air and pollution, to protect the health community and improve the areas which before the explosions, which were used for cultivation of vegetables.

NA LEONIA Lucas MAHONA


In order to edit translations, you need to log in. Log in · Register

Translation History

Google Translate
March 2, 2011
Jean MEDIA, THROUGH MTWARA FM radio SOCIAL, ENVIRONMENTAL IMPACT FROM IMEFUATILIA and explosives at Camp YALIYOLIPUKA the Tanzanian People's Army forces that 511 IN LA AREA MBOTO staff in Dar-ES-SALAAM – Large explosions inchini Tanzania bombings happened in the main warehouse kutunzia army's weapons are a country of Tanzania [TPDF] mboto staff of Dar es salaam has caused massive environmental damage. ...