Asili (Kiswahili) | Kiswahili |
---|---|
TAARIFA YA MTANDAO WA VIJANA MANISPAA YA TEMEKE KWA KIPINDI CHA UTEKELEZAJI CHA JULAY-SEPT 2009. KUTOKA: MTANDAO WA MAENDELEO YA VIJANA MANISPAA YA TEMEKE (TEYODEN) KWENDA KWA: MKURUGENZI WA HALMASHAURI MANISPAA YA TEMEKE 1.0 UTANGULIZI Temeke Youth Development Network (TEYODEN) ni Mtandao wa Maendeleo ya Vijana unaoendeshwa na vijana wenyewe miongoni mwa mitandao 19 iliyotokana na programu ya vijana nje ya shule iliyotekelezwa na Halmashauri 19 nchini Tanzania kwa ufadhili wa UNICEF. Mtandao umesajiriwa chini ya ofisi ya Makamu wa Raisi, namba ya usajiri ni OONGO/0170.TEYODEN inasimamia na kuratibu shughuli zake katika vituo 24 vya vijana vilivyopo katika kata 24 za Manispaa ya Temeke. 1.1 Dira ya TEYODEN Kuwa Mtandao bora wa Maendeleo ya vijana Tanzania unaowezesha vijana kuwajibika vya kutosha katika kubadili tabia hatarishi na kujiletea katika vituo vya vijana vya kata na asasi wanachama wa TEYODEN. 1.3 Lengo kuu la TEYODEN Kuchangia juhudi za kuleta maendeleo endelevu na thabiti ya tabia na mienendo ya vijana katika mahusiano yao hususani katika masuala ya ngono ili kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi na kutekeleza mkakati wa kupunguza umasikini ili kufikia malengoya milenia (MDG`s) 2.0 SHUGHULI ZILIZOFANYIKA • Katika miezi 3-(Julay -sept)ya utekelezaji, shughuli zifuatazo zilitekelezwa: 2.1 Utafiti kwa vijana juu ya uwajibikaji na ushiriki wa vijana katika shughuli za jamii na maendeleo. TEYODEN imefanya utafiti shirikishi kuhusu uwajibikaji na ushiriki wa vijana katika vikao vya maendeleo na shughuli za kijamii na maendeleo.Utafiti huu umetokana maoni ya The Foundation For Civil kuwa ni vyema kufanya tafiti ili kujua hali ya uwajibikaji na ushiriki wa vijana kabla ya kuwasilisha tena mradi.Matokeo ya utafiti uliofanywa kwa Mukhtasari ni kama ifuatavyo:- • 61.7% ya walengwa wa utafiti walionyesha uelewa kuhusu maana ya uwajibikaji na 38.3 % walionyesha kutoelewa maana ya uwajibikaji na dhana nzima ya uwajibikaji kwa vijana. • 50% ya walengwa walionyesha kuwa kuna uwajibikaji hafifu kwa vijana katika mitaa na kata wanakoishi na 47% ya vijana wahojiwa walisema kuwa kuna uwajibikaji wa wastani miongoni mwa vijana katika mitaa wanayoishi. • 85.3% ya vijana walisema hawashiriki katika vikao na shughuli za maendeleo ngazi ya kata na 14.7% tu ya vijana wanashiriki katika vikao na shughuli za kijamii na kimaendeleo ngazi ya kata. • 73.5% vijana waliohojiwa walisema hawashiriki vikao na shughuli za kimaendeleo ngazi ya mtaa na 26.5% walisema wanashiriki katika vikao na shughuli za kimaendeleo na jamii ngazi ya mitaa. • 67.6% ya vijana walisema hawashiriki katika shughuli za kujitolea na 32.4% za vijana walisema wanashiriki katika shughuli za kujitolea ngazi ya manispaa na kata. • 76.5% ya vijana walisema wanashiriki katika vikao vya vijana katika vituo vya kata na 23.5% wanashiriki ipasavyo katika vikao vya vituo vya vijana vya kata. • 76.5% ya vijana walihojiwa walisema vijana wanapaswa na ni muhimu sana kushiriki na kushirikishwa katika kufanya maamuzi ya kujamii na kimaendeleo,20.6% ni muhimu na 2.9% si muhimu sana kwa kuwa haina matokeo yoyote. Maazimio ya vijana kutokana na utafiti huu ni kuanzisha kwa mradi au mpango maalum utakaowezesha vijana kujua umuhimu wa uwajibikaji na ushiriki wao katika shughuli za kijamii na maendeleo.Andiko la mradi limeandikwa upya na kuwasilishwa katika ofisi za Foundation. 2.2 Mradi wa uenezaji wa sera ya vijana wa Kituo cha vijana cha makangarawe. Kituo cha vijana cha kata ya makangarawe kimeibua mradi wa kueneza sera ya vijana kwa vijana katika kata hiyo.Mradi huu umepata bahati ya kufadhiliwa na taasisi ya The Foundation For Civil Society.Mradi huu unategemewa kutekelezwa katika kipindi cha miezi 3 kuanzia mwishoni mwa Oktoba na kumalizika mwishoni mwa Disemba. 2.3 Mjadala wa vijana centre 1. Kama ilivyo kawaida kwa vijana wa TEYODEN kufanya midahalo kila jumamosi mbili katika mwezi.katika kipindi cha taarifa vijana walifanya midahalo 6 na wastani wa vijana 107 walishiriki katika midahalo hiyo. 2.4 Mafunzo ya kujenga uwezo wa Viongozi na watendaji wa TEYODEN. Katika kipindi cha taarifa viongozi na wanachama wa TEYODEN walipata nafasi ya kuhudhuria mafunzo ndani na nje ya mkoa wa Daresalaam kama ifutavyo:- 1.) Mafunzo ya uendelezaji wa Asasi za kiraia(Organisational Development) Lengo la mafunzo - Lengo la mafunzo haya ni kuinua uelewa wa wawakilishi wa asasi za kiraia kuhusu mbinu za kuendeleza asasi zao kwa kufuata mwelekeo na shughuli zenye mafanikio kwa jamii. TEYODEN ilipata nafasi ya mwakilishi mmoja katika mafunzo haya. 2.) Ushiriki wa mweka hazina wa TEYODEN katika mafunzo ya uhasibu kwa mara ya pili hoteli ya Giraffee chini ya ufadhili wa The Foundation for Civil Society. Lengo la mafunzo:- Lengo la mafunzo haya ni kuwezesha wahasibu wa asasi za kiraia kuwa na uwezo wa kuendesha shughuli za mahesabu katika Asasi zao kwa uwazi na uwajibikaji. 3.) Kikao cha wadau wa elimu ya stadi za maisha kilichofanyika hoteli ya 88 mkoa wa Morogoro. Lengo la kikao ni kupitia na kufanya marekebisho ya mwisho katika kitini cha kuwezeshea stadi za maisha kwa vijana walio nje ya shule Tanzania. TEYODEN ilipata nafasi ya kuwakilishwa na katibu mkuu katika mkutano huo. 4.) Mafunzo ya kutengeneza sabuni ya maji. Lengo la mafunzo ni kuwezesha vijana kuwa na uwezo wa kutengeneza sabuni ya maji ili kuinua kipato chao na kujiepusha na tabia hatarishi zinazoweza kuwapelekea katika maambukizi ya VVU. Katika mafunzo haya vijana 12 kutoka kata ya Vituka walipata nafasi ya kushiriki. 5.) Mafunzo ya stadi za maisha yaliyofanyika ofisi ya afisa mtendaji kata changombe. Lengo la mafunzo ni kuwezesha vijana wapatao 40 kuwa wawezeshaji wa stadi za maisha kwa vijana wenzao katika kata za Charambe,Temeke na kisarawe II. 6. Shughuli ya ufuatiliaji na usimamizi wa shughuli za vijana Manispaa ya Temeke.Katika shughuli hii taasisi za vijana 81 zilitembelewa. 2.5 Mikutano na shughuli nyingine vijana walizoshiriki. 1. Vijana 10 walishiriki katika siku ya vijana ya kimataifa katika ukumbi wa elimu ya atu wazima shughuli iliyoratibiwa na wizara ya kazi ajira na maendeleo ya vijana. 2. Ushiriki wa vijana katika vikao vya vijana ofisi za UNIC.Vijana zaidi ya 20 hushiriki katika vikao vya vijana katika kito cha habari cha umoja wa mataifa kufanya mijadala na vijana wengine nje ya Temeke. 3.Ushiriki wa vijana 4 katika mkutano wa kambi ya dunia uliofanyika kuanzia tarehe 21/7/2009 hadi 27/8/2009 katika ukumbi wa sabasaba karume hall. 3.0 KAZI ZILIZOPANGWA KUFANYIKA 3.1 TEYODEN imepanga kufanya mambo yafuatayo:- 1.) Kutekeleza mradi wa ushonaji na kudarizi kwa vijana wa kike 80 kutoka kata za Azimio,Makangarawe,Sandali na Vituka mwezi wa 12 baada ya kupata fedha kutoka ubalozi wa Ujerumani. 4.0 :HITIMISHO TEYODEN inaamini kuwa mabadiliko kwa vijana yatakayochangia maendeleo ya vijana yanawezekana kama vijana wanapewa uzito unaostahili katika kupanga, kutekeleza, kufuatilia na kutathmini shughuli za maendeleo. Viongozi wa TEYODEN na vijana siku hadi siku wamekuwa wakiongezewa uwezo katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo.Hivyo tunawashauri wadau kutumia fursa hii adimu kwa kuwatumia ili kutatua matatizo ya vijana.vijana tukijiwezesha na kuwezeshwa tunaweza. |
(Bila tafsiri) |
Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe