Base (Swahili) | English |
---|---|
@Jonathan Mulokozi (karagwe kagera Tanzania): Tutaendelea kuwa nchi masikini kwa kuwa Watanzania walio wengi ni wavivu hawataki kujishughulisha wanataka mambo ya readymade kitu kisichowezekana kwa watu wanaopenda maendeleo na wanaokataa umasikini. Ninachokiona hapa kwa viongozi wa nchi yetu wafanye kazi ya ziada ili kupambana na hii hali; kwa mfano watu asubuhi tu wako kwenye mabaa, wanacheza mabao, wamefika maofisini - wanaanza kuongelea mambo ya mipira iliyochezwa jana au itakayochezwa bila kuzingatia kitu alichoenda kukifanya pale ofisini, hivyo ombi langu kubwa Serikali yetu isichoke kuyakemea haya au ikibidi yatungiwe sheria zinazobana mambo yote yanayofanya nchi yetu kuendelea kuwa masikini. Tuchukue mifano kutoka nchi za wenzetu kama Thailand, ukifika pale mchana utafikiria nchi ile haina watu wengi - yaani asubuhi hadi saa kumi na mbili ni saa za watu kuwajibika kama maofisini, mahospitalini, viwandani, mashambani. Kuanzia hiyo saa kumi na mbili ndio watu wanaingia kwenye ujasiliamali kama; kufungua maduka (ni wakati wa shopping sasa), magenge ya vyakula (e.g. chips barabarani), hoteli za vyakula, wauzaji wa biadhaa za kila aina barabarani (huku kwetu twawaita Wamachinga) nakadhalika, yaani hawa watu wako committed kweli katika kuhakikisha kwamba njaa kwao haitajwi na kama ni mkulima anahakikisha anafungasha na mlo wake wa kumtosha anatakapokuwa huko (kitu ambacho kilifanyika miaka ya sitini huko vijijini na Tanzania yetu hii hii na mambo yakiwa yanakwenda vizuri - kijiji au mtu aliyepata njaa alikuwa ni wa kwenda shamba saa nne na kurudi nyumbani saa sita njaa inamuuma - huyu lazima umaskini nyumbani kwake utajwe na uonekane hivyo kuletea familia yake aibu mpaka hata kwa watoto wake wa kike kusababisha kutoolewa kwa kile kinachoitwa kuoa katika familia hiyo ni kukaribisha umaskini ndani ya familia nyingine. Ninamaliza kwa kuiomba tena Serikali itilie sana mkazo ikisimamia vizuri maendeleo tunayoyaona maendeleo lakini yanazidi kutupeleka kwenye umasikini, mtu yuko kwenye TV tangu asubuhi hadi jioni si kwamba ni vijana tu hata watu wazima na hasa watumishi wengi wanapokuwa hawako kazini, wanakosa mwelekeo wa maisha hivyo kushindwa hata kutunza familia na umasikini kuzidi, baa zinafunguliwa tangu asubuhi, mwajiri mchana anaita mtumishi ofisini kwake macho mekundu ananuka pombe, lakini anashindwa kukemea wakati mwingine huyo mtu kaingizwa kazi na mtu mkubwa au ni mtoto wa mkubwa, pia tumuenzi Mwalimu J.K. Nyerere ambaye hakutaka watoto wake wapewe upendeleo, watumike sawasawa inavyopaswa hata walipokuwa masomoni. TUILINDE NCHI YETU TUILILIE TANZANIA YETU kwa kuikomboa isiwe tegemezi na kulemewa kwa umasikini. |
@ Jonathan Mulokozi (Karagwe Kagera Tanzania): We will continue to be poor countries that most Tanzanians are lazy they do not want to devote to matters of readymade something impossible for people who want progress and who refuse to poverty. What I find here with the leaders of our country to work actively to combat this situation, for example the morning only are the bars, they play goals, have come to the office - they began to talk about matters of balls played yesterday or itakayochezwa without considering what he're going to do at the office, so My big request our Government isichoke kuyakemea these rules or necessary yatungiwe zinazobana things that make our country continue to be poor. Take examples from our countries as Thailand, where the day will come when that country does not think most people - even the morning until ten o'clock and two are at the people responsible as offices, hospitals, factories, farms. Starting it at ten and two are men enter into entrepreneurship as: open shops (it is during the shopping now), the steep foods (eg chips on the road), hotel food, vendors biadhaa all kinds of road (with us twawaita machinga) etc. , ie these people are committed indeed to ensure that hunger for them not itajwi and if a farmer makes sure his pack with his meal enough is entering there (something that took place sixty years in rural Tanzania planet is and what being goes well - the village or the person who received hunger was going field at four and came home at six hungry Hurt - this must be poverty in his house refer to appear so bring the family shame, until even his children's female lead kutoolewa for what is called marrying into the family is welcome reduction in other families. Completes to ask again the Government itilie much emphasis ikisimamia good progress we have seen progress but increasingly leading us to poverty, one is on TV from morning to evening is not that the youth only to adults and especially many servants when they are not reinstated, the error patterns of life that fail to keep families and poverty increase, bars zinafunguliwa since morning, the employer afternoon he called the servant in his office red eyes he stink of alcohol, but he failed to rebuke sometimes the man kaingizwa work and a great person or a child's great, too tumuenzi Mwalimu JK Nyerere, who did not want his children to be given bias, it should do the same even when they were studying. OUR COUNTRY TANZANIA TUILINDE TUILILIE redeem us, not burdened by poverty and dependency. |
Translation History
|