Base (Swahili) | English |
---|---|
BIASHARA UTOTONI NA ELIMU Mtoto Samson Hezron (11) mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya Msingi Ngh'ongh'onha katika Manispaa ya Dodoma ni miongoni mwa wanafunzi wa shule za msingi wanao juihusisha na biashara wakiwa na lengo la kusaidia kuinua kipato cha familia zao.
Samson anadai kuwa hufanya biashara kwa kufuata ratiba ya nyumbani kuwa ni lazima awe nyumbani kabla ya saa kumi na moja jioni wakati hufanya biashara kwa siku za jumamosi, jumapili, siku za mapumziko na likizo. Kijana huyu anaongeza kuwa pamoja na kufanya biashara katika umri mdogo ratiba yake ya masomo anaiheshimu na kujikuta akipata si chini ya alama 70 kwa somo la Hisabati, 80 kwa sayansi na 30 kwa somo la kiingereza. "Kiingereza ni kigumu sana kwangu; hata hivyo mwalimu wa kiingereza na sayansi Mwl. Luganissa nampenda sana kwani anaelekeza vizuri bila viboko"
Mtoto Samson nadai kuwa mtaji wake wa miwa ni kiasi cha sh 2000 ambazo humpatia faida ya kati ya sh 2000 hadi 2500 kwa siku. Kuhusu kupata muda wa kujisomea "Sam" anasema hasomi tuition kwani kaka yake anayesoma darasa la saba ana mfundisha kila siku kuanzia saa 12 jioni nyumbani kwao. Kijana Samsoni ni mmoja kati ya watoto wanaofanya biashara mbalimbali mkoani Dodoma kwa lengo la kukabiliana na hali ngumu ya maisha katika gfamilia zao. Wengi wa vijana wenye umri sawa na wa Samson hujihusisha na kuomba-omba mitaani, biashara ya vyuma chakavu na kuokota chupa za plastiki na kuziuza kwa wafanya biashara wa chupa hizo. |
Early BUSINESS AND EDUCATION Child Hezron Samson (11) fourth grade student in primary school Ngh'ongh'onha in Dodoma Municipality is among the students of primary schools who juihusisha business with the goal of helping raise the income of their families.
Samson claims that do business in accordance with a schedule of home that you must be home before ten o'clock one evening when they do business on Saturdays, Sundays, holidays and vacations. Boy adds that along with doing business at a young age his plan of study is respect and find themselves getting less than score 70 for the study of mathematics, 80 science and 30 to study English. "English is very difficult for me, though teacher English and science Mwl. Luganissa much as I love a good turn without corporal punishment "
Baby Samson claims that its capital is the amount of cane sh 2000 which gives a sh profit of between 2000 to 2500 per day. About to find time to study the "Sam" says he does not read the tuition for her brother who learns he has taught seventh grade every day starting at 12 pm at home. Boy Samson is one of the children who have various business Dodoma region in order to cope with harsh living conditions in their gfamilia. Many of the young men the same age and of Samson respond to pray-pray the street, the scrap metal business and picking up plastic bottles and selling them to merchants of these bottles. |
Translation History
|