Envaya

/M-E-D-1-1/post/9517: Kiswahili: WI00064692340E6000009517:content

Asili (Kiswahili) Kiswahili

Wanaharakati Wajadili Mchakato wa Katiba Mpya.

Mchakato wa kuandika katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unazidi kushika kasi zaidi nchini baada ya wanaharakati wa mikoa saba kukutana Dodoma kujadili na kujifunza juu ya katiba ya sasa na mapungufu yake na jinsi ya kuelimisha wananchi umuhimu wa kuwa na katiba mpya.

Warsha hiyo ya sikun tatu inafanyika katika Hoteli ya Dodoma inahudhuriwa na wawakilishi wa Mitandao ya Asasi za Kiraia kutoka katika Mikoa ya Morogoro, Lindi, Rukwa, Ruvuma, Iringa, Mbeya Dodoma na Tabora.

Washiriki wa warsha hiyo wameeleza nia yao ya kuhakikisha kuwa watadumu katika kuulinda Muungano wa Tanganyika na Zanziba na kuahidi kuwa watajitahidi kuhakikisha katika mchakato huo watajitahidi kuziondoa kasoro zinazoonekana kuwa zinayumbisha Mungano huo.

Wakichangia mada katika warsha hiyo inayoonekana kuwavuta wanaharakati ha ambao ni waumini wa Asasi za kiraia nchini wamesema kuwa kazi ya kuelimisha jamii juu ya uwepo wa Katiba Mpya ni ya muhimu inayohitaji kujituma na kuwa na moyo wa kujitolea kuisaidia jamii ili ielimke na kuwa na maamuzi yaliyo sahihi na yenye manufaa kwa Taifa.

Naye Mkufunzi wa warsha hiyo Bw. Deus Kibamba (picha ndogo)kutoka Jukwaa la Katiba amesema watanzania watashiriki kwa mara ya kwanza kutunga katiba yao kwani katiba iliyopo kwa sasa hakutungwa na watanzania bali watanzania waliletewa katiba hiyo iliyotungwa na waingereza.

Washiriki wa warsha hiyo wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kukata kiu ya watanzania katika kudai katiba mpya.

Wadau hao walisema kuwa kauli ya Rais aliyoitoa kwenye maadhimisho ya sherehe za kutimiza miaka 34 ya kuzaliwa kwa CCM mkoani Dodoma tarehe 5 Februari, 2011 ilimaliza utata uliokuwepo kutokana na kauli tata za baadhi ya watendaji wake kama Mwanacsheria Muu wa Serikali na Waziri wa Sheria na Katiba.

Warsha hiyo inayoendeshwa kwa mtindo shirikishi kwalengo la kuwafanya washiriki wote wajisikie kuwa sehemu ya mchakato huo; imekuwa ya mafanikio makubwa hasa kutokana na wengi wa washiriki kuonekana kuwa makini na wasikivu katika kila hatua.

Tanzania, Tanzania; nakupenda kwa moyo wote.... Wanaharakati waliimba wimbo huo kuonyesha mshikamano wao kwa Tanzania na nia yao njema ya kudumisha Muungano huo ambao wamesema ni wa kipekee duniani hivyo hauna budi kuendelea kuwepo ili kuiweka Tanzania katika historia hiyo.

(Bila tafsiri)

Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe