Asili (Kiswahili) | Kiswahili |
---|---|
Vijana wa Africa Upendo Group wamekuwa wakikutana mara kwa mara kujadiliana maswala mbalimbali yanayohusu vijana. kutokana na wimbi la vijana wengi ambao wanamaliza vyuo vikuu lakini kutokana na mashirika na serikali kung'ang'ania kuwa vijana hawa wawe na uzoefu katika kazi na kwa kuzingatia kuwa vijana hawa ndio kwanza wanatoka kwenye vyuo wamekuwa katika kuhangaika sana. Katika asasi yetu ya Africa Upendo Group tumekuwa na kitengo maalum cha kuwasaidia vijana kama hawa kwa kuwapatia mafunzo mbalimbali na kwa pamoja kwa njia ya kujitolea tumeweza kuwa na mikutano ya mara kwa mara.Ili kubaini njia mbadala katika kuona kuwa vijana wanapokuwa bado wapo mashuleni na baada ya kutoka wanaweza kujiajiri wenyewe kwa kufanya mambo mbalimbali yakiwemo tafiti mbalimbali.Katika kuliona hili vijana hawa wametengeneza tovuti ambayo itajulikana kama www.ICT4TD.co.tz ambayo itakuwa na shughuli mbalimbali zikiwemo vijana wengi kujitolea kufundisha masomo mbalimbali kama lugha ya kijerumani,kifaransa,Kiingereza,masomo ya Teknohama watakuwa wanajitolea zaidi katika maswala yanayohusu jamii kama usafi na utunzaji wa mazingira,Makazi au kaya,vijana walioathiriwa au wako katika hatari ya kuambukizwa UKIMWI na madawa ya kulevya n.k kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali ikiwemo Envaya,DTBI,Restless,Global Exchange,VSO wizara ya habari utamaduni na maendeleo ya vijana . Katika kutekeleza majukumu yao mbalimbali vijana wamekuwa na makongamano mbalimbali kama siku ya kujitolea duniani ambapo vijana waliweza kubadilishana uzoefu na mambo mbalimbali pia waliweza kuhudhuria mkutano ambao ulihudumiwa wa DTBI,na kwa pamoja walikutana na vijana kutoka chuo kikuu cha MIT kutoka Marekani na kubadilishana mawazo na wamekuwa wakifanya mambo mbalimbali ya mifano ya hayo. Pia wameunda Stearing commitee ambayo itakuwa na majukumu mbalimbali kwa makundi mbalimbali.Ili kuboresha zaidi na kuhakikisha kuwa vijana wanapata taarifa za msingi kutoka nje na ndani ya nchi yao.Website hii imemalizika na iko katika hatua ya kuzinduliwa karibuni. Hapa chini utaona moja ya kamati ambayo inashughulika na kuratibu makundi mbalimbali chini ya mwenyekiti wake Albert.Huyu ni kijana aliyemaliza mafunzo ya Teknohama kwenye chuo kikuu cha Dodoma na Moderator akiwa ni Neatness Msemo ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji katika Asasi hii.
kwa kukuona picha nyingi zaidi bonyeza link hapo chini: |
(Bila tafsiri) |
Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe