Asili (Kiswahili) | Kiswahili |
---|---|
Asasi ya CHACODE ni imeanzishwa na watanzania,wazalendo kwa lengo la kuunganisha nguvu kwa pamoja katika kuhakikisha ya kuwa jamii ya watanzania wanapata maendeleo.Asasi hii imeanza mchakato wake wa kimuundo mwaka 2007 baada ya wabaini changamoto za kimaendeleo zinazoikabili jamii hususan vijana kukosa ajira,wazee,wajane,watoto yatima na tatizo la ugonjwa wa UKIMWI. Makao makuu ya asasi yapo Chalinze Mkoa wa Pwani,lakini pia asasi ina ofisi ndogo katika Mkoa wa Morogoro.Imepata usajili wake mwaka 2008 baada ya kukamilisha zoezi la usajili serikali kama shirika lisilo na faida na lisilofungamana na siasa,dini au ukabila. Imesajili katika ngazi ya taifa kwa namba oongo/00002400. Malengo makuu ya asasi ni kuisaidia jamii kufikia malengo yao ya kuwa na maisha bora. Kutoa elimu na ushauri kwa makundi lengwa namna ya kuanzisha ujasiliamali na kujiongezea kipato. kusaidia jamii hususan wanawake wanaje,watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi,kuwasaidia wazee na watu wasio jiweza namna ya kutumia raslimali ndogo zilizopo ili kuhabiliana na umasikini na makali ya maisha. kuwaelimisha jamii sera na miongozo mbalimbali inayotolewa na serikali katika kujenga uelewa na taarifa sahihi zinazotolewa na serikali na kuhakikisha fursa zinazotolewa na serikali zinawanufaisha wananchi wote. Mawasiliano ni nguzo muhimu ya upatikanaji wa maendeleo hivyo,asasi ina idara ya upashanaji wa habari(media department)ambayo jukumu lake ni kuhakikisha ya kuwa wananchi wanapata taarifa sahihi za ndani na nje ya nchi kwa masilahi yao na taifa kwa ujumla. Asasi imeweza kufanikiwa kutatua migogoro ya ardhi bonde la Mikongoro katika kijiji cha Kihangaiko, Kata ya Msata Wilayani Bagamoyo. Kauli Mbiu ya asasi :Tuliona,Tukajifunza sasa tunatekeleza! |
(Bila tafsiri) |
Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe