S/N
|
SURA IBARA
|
INAVYOSOMEKA SASA
|
MAPENDEKEZO/MARE
KEBISHO
|
MAELEZO/SABABU
|
1
|
5:55:4
|
Mtoto mwenye umri chini ya miaka saba akikutwa ndani ya mipaka ya jamhuri ya muungano katika mazingira ambayo wazazi wake hawajulikani,atahesabika kuwa ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa kuzaliwa.
|
Ufanyike uchunguzi
|
Haifai kutoa uraia kwa watoto waliookotwa bila kujulikana kwani kuna hatari ya nchi nyingine kupandikiza watu wao
|
2
|
5:54:5
|
Mtoto aliye na umri wa chini ya miaka 18 ambaye wazazi wake sio raia wa Tanzania,akiasiliwa na raia wa Jamhuri ya Muungano ,kwa kuasiliwa kwake huko,kutawezesha mtoto huyo kuwa raia wa jamhuri ya Muungano wa kujiandikisha.
|
Uchunguzi ufanyike kabla ya kutoa uraia wa mtoto aliyeasiliwa
|
Kuna hatari kuwa anaweza kuletwa mtu ambaye anaweza kuhatarisha amani ya nchi.
|
3
|
6:57:1
|
Jamhuri ya muungano itakuwa na muundo wa shirikisho la serikali tatu ambazo ni :
(a)Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
(b)Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; na
(c)Serikali ya Tanzania bara.
|
Jamhuri ya Muungano itakuwa na serikali moja itakayoitwa serkali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
|
Serikali tatu zitaibua Utanganyika na Uzanzibar jambo ambalo ni hatari kwa muungano
|
|
|
|
|
|
4
|
9:105:2 b
|
Wabunge watano watakaoteuliwa na rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa za kuchaguliwa kuwa wabunge kuwakilisha watu wenye ulemavu kwa kuzingatia uwiano wa washirika wa Muungano.
|
Rais asiwachagulie watu wenye ulemavu viongozi,pia haijafafanuliwa kuwa viongozi hao watakuwa ni watu wenye ulemavu au ni watu wa kawaida
|
Kuwachagulia kundi hilo viongozi ni kuwanyima haki zao za msingi za kuchagua wawakilishi wao.
|
5
|
9:105:3
|
Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya 2(a),kila mkoa kwa upande wa Tanzania bara na wilaya kwa upande wa Zanzibar,itakuwa ni jimbo la uchaguzi.
|
Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya 2(a),kila wilaya kwa upande wa Tanzania bara na Zanzibar itakuwa jimbo la uchaguzi.
|
Haiwezekani mkoa mmoja uwe ni jimbo la uchaguzi.Kwa kufanya hivyo utashusha ufanisi wa kazi miongoni mwa wabunge.Kwa sababu wakati huu bado tuna majimbo mengi lakini ufanisi ni mdogo.
|
6
|
9:107:3
|
Bunge litasimamia serikali kwa kuangalia mwenendo wa utendaji wa raisi,makamu wa raisi,mawaziri na watendaji wakuu katika utumishi wa umma.
|
Wananchi washirikishwe katika kufuatilia utendaji wa rais,makamu wa rais na mawaziri.
|
Aliyechaguliwa na wannchi ni rais na makamu wake na si mawaziri
|
7
|
9:108:2
|
Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1)Bunge halitachukua hatua yoyote ya kitendaji ambayo,kwa desturi ni shughuli za serikali,na halitatoa maagizo yoyote ya kiutendaji kwa serikali na watumishi wa umma,isipokuwa Bunge litashauri kuhusu swala lolotelililo katika dhamana ya waziri anayehusika.
|
Mbunge awe mmoja wa waamuzi wa serikali na sio mshauri tu
|
Amechaguliwa na wanachi kuwawakilisha.Kwa kumshusha mbunge umeondoa ushiriki wa wananchi.
|
8
|
9:115:2
|
Serikali itawajibika kuyafanyia kazi mapendekezo ya Bunge kwa kadiri itakavyowezekana na kisha kuwasilisha tena bungeni hoja husika pamoja na melezo ya utekelezaji wa maelekezo ya Bunge na endapo litakataa kwa mara ya pili hoja kuhusu Bajeti ya serikali,basihoja hiyo itahesabika kuwa imepitishwa na Bunge.
|
Endapo bunge litakataa kwa maa ya pili basi maoni ya wabunge yazingatiwe kataika hoja hiyo
|
Bajeti ya serikali isipitishwe mpaka hoja hiyo itakapopitishwana bunge
|
9
|
9:116:4
|
Endapo mbunge anayetokana na chama cha siasa atapoteza sifa za kuwa mbunge kwa sababu yoyote isiyokuwa ya Bunge kumaliza muda wake,tume huru ya Uchaguzi ya Jamhuri kwa mujibu wa masharti yatakayowekwa na sheria itakayotungwa na Bunge kwa ajili hiyo itamteua na kumtangaza kuwa Mbunge mtu mwingine kutoka kwenye orodha ya majina ya wagombea iliyowasilishwa na chama hicho kwa mujibu ya Ibara ndogo ya (5)
|
Uchaguzi mdogo ufanyike kwa muda maalum
|
Tume isimchagulie mwanachi kiongozi.Kwa kufanya hivyo itakuwa inamnyima haki mwananchi ya kuchagua kiongozi.
|
10
|
9:116:5
|
Orodha ya majina ya wagombea kutoka kila chama cha siasa iliyowasilishwa kwa tume Huru ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano katika Uchaguzi mkuu ndiyo itakayoyumiwa na Tume huru ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano baada ya kushauriana na chama cha siasa kinachohusika,kwa madhumuni ya kujaza nafasi ya Mbunge inapotokea kuwa wazi,wakati wowote wa maisha ya Bunge.
|
Uchaguzi mdogo ufanyike kwa muda maalum
|
Chama cha siasa hakina mamlaka ya kuwateulia wananchi kiongozi wakishiikiana na Tume ya Uchaguzi.Wananchi ndio wenye kauli ya mwisho kuhusu mtu atakayewaongoza.
|
11,
|
7:69:3 e
|
Kumteua mwanasherua mkuu na naibu mwanasheria mkuu wa serikali
|
Kifungu kisiwepo
|
Tume maalumu yenye kuheshimu jinsia iundwe ili iweze kusaidia mchakato huru wa kuwateua waliotajwa na siyo Rais
|
12
|
4:44:1b
|
Mtu mwenye ulemavu anastahiki:
Kupata elimu kwa kutumia vifaa maalum na kushiriki katika shughuli za kijamii.
|
Somo la lugha za alama linatakiwa kuingizwa katika mitaala ya shule za msingi hadi Chuo kikuu
|
Somo la lugha za alama linatakiwa kuingizwa katika mitaala ya shule za msingi hadi Chuo kikuu
|
13
|
4:44:1f
|
Haki ya kupata ajira na kugombea nafasi za uongozi katika nyadhifa mabambali kwa usawa.
|
Haki ya kupata ajira na kugombea nafasi za uongozi katika nyadhifa mabambali kwa upendeleo.
|
Walemavu wapewe fursa za kutosha za ajira na Uongozi kwa upendeleo maalumu.
|
14
|
4:50:5
|
Ili watu wote wafaidi haki na uhuru uliotajwa katika katiba hii,kila mtu anao wajibu kutenda na kuendesha shughuli zake kwa namna ambayo haitaingilia haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.
|
Ili watu wote wafaidi haki na uhuru uliotajwa katika katiba hii,kila mtu anao wajibu kutenda na kuendesha shughuli zake kwa namna ambayo haitaingilia haki na uhuru wa watu wengine pamoja na walemavu au maslahi ya umma
|
Iongezwe pamoja na walemavu kwani walemavu hawapati haki sawa katika jamii.
|
15
|
7:83:3
|
Isipokuwa kama ataacha kushika madaraka ya Rais kutokana na kura ya kutokuwa na imani na rais,haitakuwa halali kwa mtu kumshitaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la madai dhidi ya mtualiyekuwa anashika madaraka ya Rais baada ya kuacha madaraka hayo kutokana na jambo alilofanya wakati bado anashika madaraka ya Rais.
|
Rais wa jamhuri ya muungano anaweza kuishtakiwa kwa makosa aliyoyatenda akiwa madarakani baada ya kumaliza muda wake madarakani.
|
Uwepo utaratibu wa kuwashtaki watu waliowahi kushika madaraka ya urais kwa makosa waliyoyatenda wakati wakiwa madarakani,kwani kwa kutowashtaki kunatoa mwanya kwa Rais aliyeko madarakani kufanya makosa na kuzingatia kuwa hatashitakiwa
|
16
|
7:69:3c-f
|
Akiwa kiongozi wa Serikali,Rais wa Jamhuri ya Muungano atakuwa na madaraka yafuatayo:
(c) Kuwateua Mawaziri na Naibu Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
(d) Kumteua Katibu Mkuu Kiongozi na Makatibu wakuu;
(e)kumteua mwanasheria mkuu na Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali na
(f)Kuwateua makamishna wa tume mbalimbali zilizoanzishwa kwa mujibu wa mashrti ya katiba hii
|
Akiwa kiongozi wa Serikali,Rais wa Jamhuri ya Muungano atakuwa na madaraka yafuatayo:
(c) Kuwateua Mawaziri na Naibu Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
(d) Kumteua Katibu Mkuu Kiongozi na Makatibu wakuu;
(e)kumteua mwanasheria mkuu na Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali na
(f)Kuwateua makamishna wa tume mbalimbali zilizoanzishwa kwa mujibu wa mashrti ya katiba hii kwa kushirikiana na tume maalumu ya wataalamu na bunge
|
Uteuzi huu usifanywe na rais peke yake kuwepo na utaratibu wa kushirikisha vyombo vingine katika kuthibitisha uteuzi huu kama tume maalum au Bunge.
|
17
|
7:75:c
|
Mtu atakuwa na sifa ya kuchaguliwa kushika madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ikiwa:
Angalau mmoja kati ya wazazi wake ni raia wa kuzaliwa wa jamhuri ya Muungano
|
Wazazi wote wawili wawe ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano
|
Kiongozi wa taifa anapaswa kuwa wa asili ya nchi hii na sio watu wa mchanganyiko ni hatari kwa usalama na uzalendo
|
18
|
7:75:d
|
Wakati wa kugombea ,ana umri usiopungua miaka arobaini
|
Wakati wa kugombea awe na umri usopungua miaka ishirini na tano
|
Vijana wanatengwa katika kugombea nafasi hii muhimu,uzoefu umeonyesha kuwa vijana wana uwezo mkubwa katika Nyanja za siasa na Uongozi.
|
19
|
7:84:2 b
|
Makosa makubwa ya jinai
|
Yatajwe na kuorodheshwa
|
Makosa hayo yanapaswa kufahamika ili rais ayaepuke kuyatenda na endapo akitenda kusiwepo na sintofahamu ili katiba itekelezeke kivitendo.
|