Base (Igiswayire) | Kinyarwanda |
---|---|
Ripot ya mafunzo ya kazi za mikono Vijana Simama Imara WOY Moshi Utangulizi White Orange inatekeleza mradi wa vijana simama imara. Mradi huu umefadhiliwa na SATF na una lengo la kuboresha maisha ya vijana wanoishi katika hali duni kwa kuwapa stadi za kazi na stadi za maisha. Kwa zaidi ya miezi sita WOY imekuwa ikiwafundisha vijana elimu ya kazi ya mikono ambapo wastani wa watoto 25 wamekuwa wakikutana kila jumamosi kwa ajili ya mafunzo haya. Hadi kufikia sasa VSI wamejifunza jinsi ya kutengeneza mikufu, vikuku, hereni na urembo mbalimbali kwa kutumia shanga za masai, miti na mbegu za mimea. Vile vile wamejifunza kutengeneza nyumba za asili kwa kutumia majani na udongo. Jinsi mafunzo yanavyoendeshwa Wanafunzi hujifunza kwa kuona, kuelekezwa na kutengeneza ambapo mkufunzi huleta bidhaa ambayo iliyokwisha tengenezwa au picha ya bidhaa na kisha kuaelekeza VSI jinsi ya kutengeneza (kushika uzi, sindano na jinsi ya kupangilia rangi) kisha VSI hujaribu kutengeneza na kurudia mara kwa mara hadi watakapokuwa wameelewa. Mafanikio VSI kwa kushirikia na wakufunzi wao wametengeneza bidhaa nyingi ambapo huuza katika matukio mbalimbali Malengo ya baadaye VSI wakisha kuwa na umahiri katika ufundi huu, watafundiswa sanaa nyingine ikiwemo kusuka midoli, mifuko rafiki ya mazingira na kutengeneza kadi za migomba. Wakufunzi Upendo Mkufunzi mkuu Jema Mkufunzi Msaidizi Mrs Nyata- Bibi Taarifa ya mafunzo ya uongozi yaliyotolewa kwa VSI katika ukumbi wa ofisi ya WOY Moshi Utangulizi Kwa msaada kutoka SATF White Orange Youth wanatekeleza mradi unaitwa ‘Vijana Simam Imara’ Mradi huu umeanzishwa kwa kujifunza mafanikio ya mfano kwa shirika la Humuliza linalopatikana kanda ya ziwa Victoria. Shughuli ambazo WOY wanafanya katika mradi huu ni pamoja na kuwafundisha vijana elimu ya uongozi na stadi za maisha Katika mwezi wa Mei WOY ilifanya mafunzo ya Stadi za maisha na Uongozi kwa VSI. Mafunzo haya yalifanyika kwa muda wa siku tatu ambapo jumla ya watoto 26 waliudhuria. Mafunzo haya yalifanyika katika ofisi za WOY zilizopo majengo. Lengo la mafunzo Mafunzo haya yalilenga kuwajengea uelewa VSI kueliwa maana ya uongozi, aina mbalimbali za uongozi na sifa za kiongozi bora. Mwezeshaji alielezea kwamba uongozi ni dhana ambayo humpa mtu dhamana ya kutawala au kuongoza watu au makundi Fulani pia alielezea kwamba uongozi/viongozi wapo wa aina mbalimbali kama wafuavyo • Viongozi wa kuchaguliwa- Ilielezewa kwamba viongozi wakuchaguliwa huchaguliwa na watu. aidha kwa kutumia kura au chaguzi za watu kutokana na sababu zao • Viongozi wa kuteuliwa- Ilielezewa kwamba aoina hii ya uongozi, viongozi husika huteuiwa kutokana na mamlaka mbalimbali kwa mfano wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa ambao huteuliwa na mamlaka za juu za serikali aidha kutokana na uzoefu wao wa muda mrefu au kutokana na sababu nyinginzo muhimu. Mwezeshaji alielezea kwamba zipo aina mbalimbali za uongozi kama ifutavyoongozi wa Uongozi wa kidemokrasia Ilielezwa kwamba uongozi wa kidemokrasia ni ule unaopatikana kwa njia ya kidemokrasia na kwamba njia pekee ya kupata uongozi/viongozi ni kwa kufanya uchaguzi uio huru na haki. Pia uongozi wa kidemokrasia unaweza kupatikana kwa kuteuliwa na viongozi waliochaguliwa kidemokrasia kama zinavyoeleza katiba na sheria za nchi. Uongozi wa kidikteta Mwezeshaji alielezea kwamba uongozi wa kidikteta ni ule unaopatikana kwa kutumia mabavu. Njia hizi ni pamoja na zile za kufanya mapinduzi ya kijeshi. Kadhalika kiongozi anaweza kupatikana kwa njia ya uchaguzi wa kidemorasia lakini baadaye akawa hatawali kwa kufuata misingi ya kidemokrasia ikiwa ni pamoja na kutofuata sheria, kanuni, taratibu na sheria zilizopo. Mwezeshaji aliwaeezea washiriki kwamba kiongozi anatakiwa awe na sifambalimbali ambazo ndizo zinazomwezesha kukubalika na watu au makundi aya watu anayowaongoza katika ngazi mabalimbali. Sifa hizo zilielezewa kama ifuatavyo: 1. Anapaswa awe muwazi 2 .Anapaswa awe mwenyekuheshimu mawazo ya watu wengine 3 .Anapaswa awe mwaminifu 4 .Anayekubalika katika jamii 5 .Awe na uwezo wa kupngoza 6 .Awe mkweli na 7 .Akubali kukusolewa na 8 .Asiwe na jazba Baada ya kuwasilisha somo hili la uwongozi, mwezeshaji aliwaelezea washiriki kwamba, ili kuwa kiongozi bora ni lazima kuzingatia sifa tajwa hapo juu ili aweze kukubaika na watu au mamlaka mbalimbali. Baada ya somo hili kumalizika washiriki waliuliza maswali mbalimbali ambayo yalijibiwa. Washiriki waliitimisha kwa kusema kwamba somo limeeleweka na kufuata sifa hizo ili wawe viongozi bora wa siku zijazo. Igizo Watoto waligawanywa katika makundi mawili, kundi A lilifanya igizo la uongozi usio bora, na kundi B likafanya igizo la uongozi bora. Baada ya maigizo haya mwezeshaji alianzisha mjadala kwa kuuliza maswali watoto kwamba ni uongozi gani wangeupenda na ni sababu zipi zilizowafanya wapende aina hiyo ya uongozi. Wawezeshaji Raphael Waitta Gamaliel Mbaase Orodha ya washiriki 1. Mwanahawa M Shayo 2. Mwajuma Bakari 3. Mariamu juma 4. Halima Hashimu 5. Zainabuu Hashimu 6. Magreth Robinson 7. Aviti Mustafa 8. Anjiti Mustafa 9. Niteshi Mustafa 10. Rashidi Issa. 11. Deo Frank 12. Japhet Yohana 13. Stivin Dobald 14. Merry stephano 15. Josephine JAMES 16. John Godfrey 17. Athumani Gabon 18. Mapinduzi Ally 19. Bakari hasani 20. Hamza Mudy 21. Lydia Joseph 22. Elizabeth Gasper 23. Amani Raphael 24. Swahumu Isa 25. Merry Stephano 26. Lillian Alex |
(Not translated) |
Kugirango ugire icyo uhindura kubyo wasemuye, ugomba kwinjira mu rubuga Injira · Iyandikishe