Base (Swahili) | English | |||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
UNITED AFRICANS SHIRIKA LA UMOJA WA WATU WA AFRIKA APAPO MAANA YA APAPO APAPO ni shirika la umoja wa watu wa Afrika lenye lengo la kushirikiana na serikari za Mataifa ulimwenguni katika kuleta mageuzi kwa kupambana,kuzuia na kuondoa changamoto ndani ya jamii zilizoainishwa katika Azimio la Umoja wa Mataifa namba 102 la mwaka 1952. KIFUPISHO CHA APAPO APAPO ni kifupisho cha African Poor And Patient Organization. KUANZISHWA KWA APAPO Shirika la APAPO lilianzishwa kwa sheria namba 24 ya mwaka 2002 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa usajili Na.00005441 mnamo April 4, 2012. MADHUMUNI YA KUANZISHA APAPO Dhumuni la kuanzishwa APAPO lilitokana na waasisi wake kufanya utafiti dhidi ya chimbuko na suluhu la umaskini,ujinga na maradhi duniani. LENGO KUU LA KUANZISHA SHIRIKA LA APAPO Lengo kuu la kuanzisha APAPO ni kushirikiana na kuziunga mkono serikali katika kuleta mageuzi kwa kupambana, kuzuia na kuondoa changamoto zinazoikabili au ambazo zingeikabili jamii. DIRA Dira ya Shirika Tukufu la APAPO ni kuwa kioo cha Huduma za Afya, Elimu, Ulinzi na Usalama , Usawa wa Kijinsia, Kijamii, Kiuchumi na Kiutamaduni duniani. DHAMIRA Dhamira ya Shirika ni kuhakikisha kuwa rasilimali zilizopo zinatumika barabara katika kupambana, kuzuia na kuondoa ujinga, maradhi na umaskini ndani ya jamii. MUDA NA MAENEO YA UTAFITI KABLA YA KUANZISHWA APAPO Utafiti wa kubaini chimbuko na suluhu la umaskini, ujinga na maradhi ulianza mnamo Julai 1998 katika misitu ya Itanonge, Katuma Mkoani Katavi nchini Tanzania na kuendelea katika nchi mbalimbali duniani na kumalizika mnamo Julai 2010 katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas nchini Uingereza. MUDA NA MAENEO YA UCHUNGUZI AU MAFUNZO (Field) KABLA YA SHUGHULI RASMI ZA SHIRIKA Kutokana na ukweli usiopingika usemao kuwa ‘Kabla ya kufungua Mradi Chunguza’ falsafa hii ilimfanya Gavana wa shirika baada ya usajili na kabla ya kuzindua miradi mbalimbali ikiwamo usajili wanachama wa APAPO, alichukua fursa kutembelea mikoa mbalimbali nchini Tanzania kwa ajili ya kulinadi shirika na kutafuta wajumbe au wawakilishi wa shirika watakaoliwakilisha shirika katika nchi na mikoa mbalimbali. Pamoja na mkoa wa Dar Es Salaam alipoweka kambi katika eneo la ubungo Msewe kwa kufungua ofisi ya muda kwa miezi minane kwa ajili ya kushirikiana na serikali kuu kwa urahisi na uhakika na kupata wajumbe mkoani humo. Aidha alizulu pia mikoa ya Morogoro,Iringa, Mbeya, Rukwa, Katavi, Kigoma na Tabora kabla ya kurudi katika nafasi yake na kuanza shughuli rasmi baada ya kubaini changamoto zinazoendelea ndani ya jamii. CHIMBUKO LA UMASKINI, UJINGA NA MARADHI NDANI YA JAMII Matokeo ya utafiti yalionesha kuwa pamoja na vyanzo mbalimbali vinavyosababisha umaskini,ujinga na maradhi ndani ya jamii,ukiwemo ukosefu wa imani, matumaini, subira, uvumilivu na uadilifu,chanzo kikubwa kabisa ni wananchi hasa wanaoishi maisha ya chini kukosa maarifa, umoja, mshikamano na ushirikiano hususani kabla na wakati wa matatizo miongoni mwao wakinung’unika, wakilaumu, wakisubiri na kutegemea serikali kuondoa changamoto zinazoweza kuondolewa na wao wenyewe. NCHI WANACHAMA WA APAPO Shirika la APAPO ni la kimataifa lenye nchi wanachama wa nchi zote barani Afrika, ambalo linasambaa kwa kasi kubwa sana ili kuwafikia wananchi wote hasa waishio maisha ya chini na baadaye kuenea dunia nzima kama Dira ya Shirika ukilinganisha na muda wa kuzaliwa kwake. KANDA ZA SHIRIKA Shirika limegawanyika katika Kanda sita(6) za Afrika ambazo ni:-
HUDUMA ZA SHIRIKA Shirika linatoa Huduma mbalimbali kwa jamii kama zilivyoorodheshwa hapo chini:-
Huduma za Jumla Huduma hizi zinatolewa au zitatolewa kwa jamii nzima bila kujali kuwa mwananchi ni mwanachama au la. Usajili wa Wanachama kwa hiari; .Kutoa Ajira kwa Vijana na Wastaafu; Kuzuia Ajali na Majeruhi au Vifo vitokanavyo na Ajali; Kuzuia Virusi vya Ukimwi na Ukimwi; Kutoa Msaada wa Matibabu ya Rufaa na yasio ya Rufaa, Elimu ya Chekechea, Msingi, Sekondari na Chuo kwa Mayatima,Wakimbizi, watoto wa walemavu na watu maskini
Kutoa Msaada wa chakula, mavazi na malazi kwa wahanga wa njaa, vita,Maafa na Majanga; Kusimamia Mazingira,Sheria,Wajibu, Haki za Binadamu na Usafiri wa nchi kavu na majini; Kuyasaidia Mashirika ya Kiserikali na yasio ya Kiserikali yanayotoa huduma zinazofanana na shirika mama na kutoa Elimu ya Wema na Ubaya kwa Watoto na Vijana ikiwa ni kuwaandaa Kiroho, Kimwili, Kiakili, Kisaikolojia, Kijamii, Kiuchumi na Kiutamaduni ili kuzuia, kupambana, Kukabiliana na Kushinda changamoto ambazo zinaikabili au zingeikabili jamii.
SHUGHULI KUBWA YA APAPO Shughuli kubwa ya APAPO ni kuwaelimisha wananchi ili wajitambue, waamke, waungane, wajitegemee na wajiajiri kwa kutumia lasirimali walizonazo pamoja na vyanzo vingine vya Mapato ya Shirika katika kujiinua kiuchumi na kujikomboa dhidi ya umaskini, ujinga na maradhi miongoni mwao badala ya kubweteka, kunung’unika, kulaumu na kusubiri serikali zenye kuelemewa na mizigo mikubwa na hivyo kushindwa kumudu mahitaji mengine ya wananchi kwa wakati. MAJUKUMU NA WAJIBU WA VIONGOZI NA WATENDAJI WA SERIKALI ZA MITAA KWA SHIRIKA Pamoja na Sera ya Taifa ya Ajira 2008 inayobainisha Majukumu na Wajibu wa kila mdau, ili kufikia lengo lililokusudiwa ikiwa ni pamoja na kupunguza au kuondoa tatizo la ukosefu wa Ajira na viwango vya ajira isiyokidhi kiwango, Viongozi na Watendaji wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa watakuwa na wajibu ufuatao kwa Shirika:- · Kushirikishana na kushirikiana bila kuingiliana wala kupingana katika kuielimisha jamii juu ya utumiaji wa rasilimali walizonazo na kutumia fursa zilizopo ili kuondokana na tatizo la umaskini wa mawazo na kipato na kuweka wazi mipaka ya uwajibikaji; Kulitambulisha Shirika katika ngazi zingine za Utawala kwa wakati; · Kutoa ushauri wa mara kwa mara katika utekelezaji wa majukumu yake ili kuleta tija katika jamii; · Kufuatilia na kusambaza taarifa za shirika kwa jamii nzima; · Kufanya Ubia na Shirika kwa kutoa fursa ya kutumia ofisi za serikali za mitaa ngazi ya mtaa/kijiji kuwa vituo vya Huduma za Shirika kwa wananchi wa maeneo husika ikiwa ni pamoja na Uandikishaji Wanachama wa Shirika, Mayatima, Wazee, Walemavu na wagonjwa wa muda mrefu wasio na kipato; · Viongozi wa ngazi zote (mfano Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa/kijiji) kukubali kuwa walezi wa Shirika ngazi husika watakaohudhuria vikao vya Kamati za Uongozi wa shirika kila mwezi kikatiba, kuwashauri viongozi wa shirika na kuhakikisha utekelezaji wa mpango huu kwa jamii ya eneo husika.
SEMINA ELEKEZI KWA VIONGOZI NA WATENDAJI WA SERIKALI ZA MITAA Kwa mujibu wa kanuni za ushirikishaji wa wadau wengine wa Maendeleo, Maofisa wa shirika wana wajibu wa kutoa Semina Elekezi endelevu kila inapobidi kwa viongozi na watendaji wa Serikali za Mitaa wenye lengo la kushirikiana na kuliunga mkono Shirika katika utekelezaji wa majukumu ili kuwapa uelewa wa shughuli na Huduma za Shirika kwa jamii wanayoiongoza .
KAULI MBIU 1. KAULI MBIU YA MPANGO “Wananchi, Tuungane Tujitegemee” 2. KAULI MBIU YA AJIRA “Wajibu na Haki “
MAWASILIANO KAMISHINA WA SHIRIKA...............................................................................................+255764876045 BARUA PEPE: apapoafrica@gmail.com TOVUTI: WWW. Envaya.org/apapo
|
UNITED AFRICANS ORGANISATION OF THE PEOPLE OF AFRICAN UNITY APAPO MEANING OF APAPO APAPO is an union of the peoples of Africa with the aim of cooperating with governments of nations in the world in transforming the fight, prevent and eliminate domestic social challenges outlined in the UN Declaration of number 102 of the year 1952. An acronym of APAPO APAPO is an acronym of the African Poor And Patient Organization. ESTABLISHMENT OF APAPO APAPO agency created by Act No. 24 of 2002 of the United Republic of Tanzania for registration Na.00005441 on April 4, 2012. PURPOSE OF ESTABLISHING APAPO The purpose of the establishment APAPO attributed to the founders of doing research from the source and the solution to poverty, ignorance and disease around the world. MAJOR GOAL OF DEVELOPING CORPORATION APAPO The main objective of establishing APAPO is cooperating with the government in supporting reforms to combat, prevent and eliminate challenges which facing or could face society. VISION Vision of APAPO Noble Corporation is a mirror of Health Services, Education, Defence and Security, Gender Equality, Social, Economic and Cultural in the world. MISSION Corporate mission is to ensure that available resources are used properly to combat, prevent and eliminate ignorance, disease and poverty in the community. LONG AND AREAS OF RESEARCH BEFORE THE ESTABLISHMENT APAPO Research to identify the source and the solution to poverty, ignorance and disease began in July 1998 into the forests of Itanonge, Katuma -Katavi in Tanzania and continued in various countries and ended in July 2010 at St. Thomas Hospital in England. LONG AND AREAS OF CASE OR TRAINING (Field) BEFORE THE OFFICIAL ACTIVITIES OF ORGANIZATION Due to a fact saying that "Before opening the Project Explore 'this philosophy made him governor of the corporation after the registration and re-launch various projects including the registration members of APAPO, took the opportunity to visit various regions in Tanzania for spreading organization for seeking members to work or represent the organization in various countries and regions. Despite Dar Es Salaam where he encamped at the Ubungo Msewe for eight months for cooperating with the central government simply sure to get members in the region, he visited also regions of Morogoro, Iringa, Mbeya, Rukwa , Katavi, Kigoma and Tabora before returning into place and start registering official members shall comprise the Executive Committee or the Governing after identifying ongoing challenges within the community. Causes of poverty, ignorance and disease within the community Results of the study showed that despite the underlying causes of poverty, ignorance and disease in the community, including a lack of knowledge,faith, hope, patience, perseverance and integrity, a major source size is the people, especially those living under a lack of unity, solidarity and cooperation, especially before and when the disease problems, especially if they murmured among themselves, they complain, waiting and relying on the government to remove the challenges that can be removed by themselves. COUNTRY MEMBERS OF APAPO Organization is an international APAPO-member of all countries in Africa, which spreads very rapidly to reach all citizens, especially rural life down and then spread the whole world as Vision Corporation compared to the time of its formation. ZONES OF ORGANISATION The organization is divided into six zones (6) of Africa, namely: -
East African Provinces East African provinces are Burundi, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Sudan, South Sudan, Somalia, Tanzania and Uganda.
|
Translation History
|