Envaya

Ubusobanuro: English (en): User Content: WI000CDC1E53CF1000007180:content

Base (Icyongereza) English
Community Organization for Life and Development "COLD" ni asasi isiyokuwa ya faida, ilianzishwa 26 Novemba 2008 katika kijiji cha Buyange, wilaya ya Kahama, Tanzania. Ilisajiliwa 28 Mei 2009 na kupewa hati yenye namba za usajili KHM/CBO/95. Inafanya kazi ya kutetea haki za watoto Tanzania. Ni dhahiri kuwa matatizo ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu yanazidi kuongezeka kila kuchapo, kundi hili la watoto limekuwa likiwekwa pembezoni, likipuuzwa na kunyanyaswa. Hali hii imewafanya watoto kukimbilia ajira za ama majumbani au migodini, kushiriki katika ama uuzaji au utumiaji wa madawa ya kulevya, ulevi na kujiingiza katika biashara ya mapenzi katika umri mdogo. Matatizo haya yanawaweka katika mazingira tata, rahisi kuambukizwa magonjwa kama vile VVU/UKIMWI. Imetafitiwa na kuthibitishwa kuwa jitihada za mashirika ya kiserikali, mashirika ya kidini na mashirika yasiyo ya kiserikali kuondoa matatizo ya watoto walio katika hatari zinahitaji msaada wa ziada kutoka katika jamii husika. COLD inashirikiana na jamii kuboresha maisha. Kupitia ushirikiano huu, jamii inapata ufahamu na rasilimali zinazohitajika kuboresha maisha ya watoto na kuushinda umaskini. Asasi imefanikiwa kuwabaini watoto yatima na walio katika mazingira magumu 669 katika eneo la utekelezaji, kutoa sare za shule doti 55 kwa watoto yatima 55 wanaosoma katika shule za msingi za Bugarama, Buyange na Ibanza na kuendesha mafunzo juu ya kujikinga na maambukizi ya VVU/UKIMWI, ushauri nasaha na stadi za maisha kwa watoto 110 wa shule za msingi za Bugarama na Ibanza.
(Not translated)

Kugirango ugire icyo uhindura kubyo wasemuye, ugomba kwinjira mu rubuga Injira · Iyandikishe