Asili (Kiswahili) | English |
---|---|
Napenda kutumia nafasi hii kuwapongeza wana-Kikundi cha Waishio na Virusi vya UKIMWI cha Kitangari kwa ujasiri wenu wa kujitambulisha kwa jamii kwamba mmepata maambukizo ya virusi vya UKIMWI na kwamba sasa mnaishi kwa matumaini. Napenda kuwahamasisha kwa kusema kwamba; kujitambua kwamba umeambukizwa virusi vya UKIMWI ni hatua moja muhimu ya kuongeza siku zako za kuishi, kuliko yule ambaye hajui kama ameambukizwa au la! Ukijitambua ni rahisi kuchukua tahadhari. Hivyo naomba mpokee elimu ifuatayo:- 1. Epuka kabisa kujiongezea virusi vingine. Pambana na hivyo hivyo virusi ulivyonavyo mwilini. Wapo waliojali afya zao na ambao Mungu amewajalia wameweza, kuishi miaka mingi bila kukabiliwa na matatizo makubwa. Njia ya mkato ya kujiongezea virusi vingine ni kwa kuendekeza ngono zisizo salama wakati unajua kuwa umeathirika. Wakati wote hakikisha unafanya ngono salama kama ni lazima. Tumia kondom. 2. Kila mwathirika ahakikishe ana miti michache ya mipapai ili kumwezesha kupata matunda kwa urahisi. Nimetaja mipapai kutokana na urahisi wake wa kuipata na kupanda, pia haina gharama. Kumbuka kuwa ni muhimu kwa mwathirika kuhakikisha kuwa kila mlo wake mboga za majani na matunda yanakuwepo kila siku. Kama unaweza kula matunda mengi kisha chakula kiasi ni vizuri sana kwako. Tiba ya kwanza kwa mwathirika ni kwa kula matunda na mboga za majani kwa wingi, ndipo zinafuata dawa. 3. Ni muhimu kikundi kikawa na miradi midogo midogo itakayowaingizia fedha. Kwa sehemu kubwa unyanyapaa unachagizwa sana na umaskini tulionao. Waathirika wenye uwezo wa kifedha, jamii inawaheshimu licha ya kujua kuwa wameathirika. Kuanzisha miradi si lazima uwe na maelfu ya fedha, moja ya majukumu ya Taasisi ya Kupambana na UKIMWI ni pamoja na kutoa elimu ya namna ya kuendesha miradi kwa vikundi kama hivyo. 4. Kama una familia kwa maana ya watoto; wanaosoma au wanaotarajiwa kuanza shule, kila mmoja wenu ahakikishe anakuwa na mpango mkakati wa kuwapatia watoto wake elimu. Hakuna ukombozi ambao ni muhimu katika maisha ambao unaoweza kulinganishwa na elimu. Elimu ni kila kitu. Wakati huu ambapo unamudu kufanya shughuli mbali mbali ni vyema kuelekeza nguvu zako katika kuwasomesha watoto wako hadi wafikie elimu ya juu. Elimu nzuri itamjengea mtoto wako mazingira mazuri ya kupata ajira. Mtoto akipata ajira, familia nzima itakuwa na uhakika wa maisha. |
Let me use this opportunity to congratulate the children-group living with HIV Kitangari of your courage to introduce yourself to the community that you have HIV infection now that you live in hope. I would like to say that motivate, recognize that you are infected with HIV is one important step to increase your days of life, than one who does not know if he is infected or not! Ukijitambua is easy to take precautions. So I receive the following knowledge: - ,, 1. Avoid quite add other viruses. Struggle with the same virus that they have the body. There are those who care about their health and that God has granted they can live many years without facing serious problems. Shortcut to add other viruses are adapted to unprotected sex when you know that you are infected. Always make sure you practice safe sex if necessary. Use condoms. ,, 2. Each victim should make sure he has a couple of papaya trees in order to get the fruit easily. Cites papaya due to its ease of access and climbing, it also has costs. Remember that it is important for the victim to ensure that every meal fresh vegetables and fruits readily available every day. If you can eat so many fruits and food is very good for you. Treatment of the first victim is to eat fruits and vegetables in bulk, then follow the medication. ,, 3. It became important group and small projects itakayowaingizia money. For the most part they are instructed to stigma and poverty we have. Victims who have financial capacity, community inawaheshimu despite knowing that they are infected. Setup projects do not necessarily have thousands of silver, one of the functions of the Institute for AIDS include providing education on how to run projects for such groups. ,, 4. If you have a family for the children who read or are expected to start school, make sure everyone has a strategic plan to give his children education. No redemption which is important in life that you can compare and education. Education is everything. At this time when you can afford to do different activities should focus your energy on your kids manage to achieve higher education. Education itamjengea good environment for your child to get jobs. Baby's got a job, the whole family will be assured of life. |
Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe
Historia ya tafsiri
|