tosa inafanya kazi katika shule za msingi kwa kushirikiana na waalimu na viongozi wa mitaa ili kupata habari sahihi kuhusu watoto wanaohitaji kufadhiliwa na shirika letu
tosa pia inafanya uchunguzi ili kujua wahitaji walio na hali ngumu zaidi na kuwapa kipaumbele.pia inafatilia afya za watoto hao kwa karibu na mahitaji ya chakula inapotokea uhitaji huu.
tosa inatajia kuwasiliana na RITA ili watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira hatarishi wasajiliwe ili wapewe vyeti vya kuzaliwa.
kuendelea na kampeni za malaria kwa kufanya matamasha katika shule za msingi na kugawa vyandarua kwa wajane,watoto yatima na jamii zenye kipato kidogo
kuendelea kuwaelimisha jamii juu ya haki za wajane na watototo yatima kwa kupitia
vipeperushi,mikutano,makongamano na vyombo vya habari.