Envaya
Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

TARUCODEFU ni kifupi cha Tambani Rural Community Development Fund, ni Asasi isiyo kuwa ya kiserikali na isiyokuwa ya kupata faida, imesajiliwa mwaka 2001 na kupata hati na SO 10944, Asasi hii inafanya kazi zake katika mikoa ya Pwani, Mtwara na Lindi, ambapo makao makuu yake yapo katika wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani. Nembo ya asasi hii ni picha inayo onyesha mtu analima kwa kutumia trekta na juu yake yamepita maandishi ya duara yanayo someka TARUCODEFU.