Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

ELIMU YA UKIMWI SEKONDARI NA VYUONI INASAHAULIKA.

Ng'onye John (Taasisi ya Kupambana na Ukimwi Kitangari- Newala.)
June 30, 2011 at 10:00 AM EAT

Napenda kueleza machahche kuhusiana na Hali ilivyo kuhusu HIV/AIDS kwenye shule za Sekondari na Vyuo mbalimbali vya Ualimu hapa nchini Tanzania.

Nazungumzia jambo hili kwa sababu msisitizo kwa Vijana hawa upo kwenye Elimu ya Compyuta na Masomo ya Sayansi, lakini HIV/AIDS haihusishwi. Kutohusishwa inaonekana hawajengewi moyo wa Maisha ya Baadae,jambo ambalo mara wanapofuzu Taaluma yao wanaonekana tayari wana VVU lakini pia hawapendi kupangiwa kazi maeneo ya Mbali na mjini kwani wengine wanajihisi vibaya na hali wakiyonayo. Hii ipo sambamba na magonjwa ya zinaa kwani KITU MAPENZI kinawasumbua sana vijana hawa.

Ninachoshauri Mashirika mbalimbali, Walimu wa Ushauri nasaha na Wataalamu wengine wa Afya fanyeni juhudi za Makusudi ili Rika hili wawe na Subira ya Mapenzi kwani kila jambo lipo mbele yao.

bopniphace john bupolo (mtcd)
July 2, 2011 at 12:10 PM EAT (edited March 26, 2012 at 8:06 AM EAT)

@Ng'onye John (Taasisi ya Kupambana na Ukimwi Kitangari- Newala.): Nafikili jambo lakufanya viongozi wa dini, wanasiasa na walimu iwe kauli mbiu kwao wanapokuwa wako jukwaani iwe salamu yao kwa hadhira, asante!

[message deleted]
AUGUSTINE J.NYAKATOMA (MWANZA TANZANIA)
July 26, 2011 at 8:39 AM EAT (edited March 26, 2012 at 8:06 AM EAT)

Phytza@yahoo.com (Peace and Hope for Youth Development "PHY")

Dhana ya kutowajali vijana hasa wa vyuo mbalimbali hasa vyuo vya elimu ya juu katika suala zima la  Ukimwi, kwakuwa jamii inaamini kuwa vijana hawa wana uelewa kuhusu UKIMWI na madhara yake, kitu ambacho kwa mtazamo wangu sio sahihi. Hivyo nadhani vijana wa elimu ya sekondari na vyuo vya elimu ya juu wanapaswa kuelimishwa pia stadi za maisha ili kupata elimu ya kujithamini, na hivyo kuepuka kupoteza watalaamu katika fani mbalimbali kwa njia ya UKIMWI.


Add New Message

Invite people to participate