Napenda kuwasalimuni wote wanaharakati na wadau wote wapenda maendeleo ya Elimu Tanzania. Leo katika nafasi hii napenda kuuliza kwamba katika mafunzo ya Ualimu siku hizi ile Syllabus iliyokuwa inashughulikia Masomo ya Kusoma,kuandika na kuhesabu imefutwa kwenye vyuo vya Ualimu?
Nauliza hivyo kwasababu wanachuo wa vyuo vya Ualimu wanapokwenda kufanya mazoezi ya kufundisha wote hupenda kufundisha kuanzia DRS III hadi VII tu, lakini darasa la I na II hawapendi kufanya mazoezi ya kufundisha NAOMBA UFAFANUZI KWENU WATALAAMU.