Tarehe 21 hadi 23 Nov.2011 Asasi ta TAKUUKI imepata nafasi kushiriki Tamasha la 9 la azaki bora Tanzania ambalo limefanyika Dar es Salaam katika Hoteli ya Blue Peal.Mwakilishi wa Azaki amejionea mwenyewe jinsi asasi mbalimbali walivyoweza kuonesha kazi zao ambazo wanahudumia jamii.Mwakilishi wa asasi hiyo ambaye ni Mkurugenzi wa TAKUUKI amefurahishwa sana kujionea machapisho na vitabu mbalimbali ambavyo vina Elimu Mzuri na aina mbalimbali ya ujumbe kwa jamii.Mfano Asasi ya TACOSODE imetoa kitini cha Kitaifa cha kufundishia mbinu na njia za ufundishaji,asasi ya ZAFELA ya Zanzibar imetoa kipeperushi cha Stadi za Maisha,asasi ya DEL MUNDO kwa ushirikiano wa wilaya ya Same na Singida wametoa vipeperushi vya Uzazi na Ujinsia na asasi ya SAIDIA WAZEE KARAGWE nao wametoa kipeperushi kinachoonesha shughuli mbalimbali ambazo zinasaidia wazee kuondokana na umaskini na asasi zingine zimeonesha machapisho safi na mazuri kiasi kwamba siwezi kutaja zote, hii imeonesha wazi kwamba asasi zipo karibu kabisa na jamii na ndizo zinafahamu moja kwa moja mwanajamii anahitaji nini ili kujua afanye nini,aende wapi ili kuondokana na umaskini.Mwakilishi wa TAKUUKI amepata mambo mengi amabayo maonesho yajayo aone anaanza na nini.Hongera sana wana Azaki. Hata hivyo pongezi za Pekee kabisa kwa The Foundation For Civil Society kufanikisha maandalizi yote haya muhimu.
November 23, 2011